Ujasiri katika maisha yetu
Katika maisha tunapitia mambo mengi sana, na kuna kipindi mtu waweza jikuta katika mitihani ya kila aina na kupitia mitihani hiyo watu wengi hufikia hatua ya kukata tamaa na kusahau kabisa ndoto zao.
Kila mtu kajaliwa kipaji, na hapa nadiriki kusema hakuna binadamu ambaye amezaliwa bila ya kuwa na kipawa cha kufanya kitu fulani.
Wengi tumetofautiana na jinsi tunavyo yachukulia mambo, kukatishwa tamaa kidogo tu kwaweza kumfanya mtu abadili wazo lake la awali na kuja na kitu tofauti ambacho hakina ladha ya awali.
Ili kuweza kufanikisha mambo yetu twatakiwa kuwa na msimamo wenye maono ya baadae na kushika kazi zetu kwa mapenzi ya ukweli na kila kitakacho letwa kama maoni basi tuvitumie katika kuboresha kazi zetu.
Kuna wakati unatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili uweze kuamsha kipaji chako na kuifanya kuwa fursa ya wewe kuishi na baadae kuja kutuletea faida na hata ajira.
Maisha ni kuwa mbunifu na kutokata tamaa.

0 comments: