Unaposema huyu binti kicheche,........

19:14:00 Unknown 0 Comments

Fuledi na kidele ni marafiki walioishi kwa miaka mingi wakifanya kazi na kusaidia kwa kila jambo lililolenga kuyafanikisha maisha yao na kuwa ya furaha.

Mwaka mmoja uliopita waligombana katika ugomvi ambao hata wao naamini hawajui nini kilikuwa chanzo cha kuzuka ugomvi huo.

Baada ya ugomvi huo waligeuka na kuwa maadau zaidi ya paka na panya. Lakini Fuledi ndiye aliyekuwa mkorofi, kwani kila maraalizusha maneno ambayo kila mtu aliyeyasikia yalimuuma sana, kwani alifikia hatua ya kumpakazia maneno yasiyostahili kusemwa hadharani.

Ikafikia kipindi Fuledi akaanza kukumbuka ule urafiki wao na baadhi ya watu wenye busara wakawa wakimshauri juu ya kuyamaliza mambo hayo.

Fuledi maneno yale yalimwingia na kujikuta akimsaka kidele ili wayamalize na kuwa marafiki tena, kidele ambaye alishayazoea maneno yale na ule uhasama ambao haukumpa usingizi kwa muda pamoja na kejeli kem kem alizokuwa akitupiwa mtaani hasa baada ya yale maneno alitabasamu na kisha kusema .

"Fuledi nimekubali kukusamehe, ila nitaomba kabla sijakusamehe kabisa basi kuna jambo ulifanye" Fuledi akakubali.

Kidele akaingia ndani na kurudi na kuku aliye hai na kumwomba fuledi amachukue na kumnyonyoa nyoya moja moja huku akipita barabarani.

Fuledi akaona ni kazi rahisi, akamchukua yule kuku na kuanza kazi ile ya kunyonyoa huku kuku yule akipiga kelele na kisha akamaliza.

Baada ya kumaliza Fuledi alirudi kwa kidele ili wayamalize, kidele akasema bado jambo la mwisho. "Naomba ukayaokote tena yale manyoyana kuja nayo".

Fuledi alienda na kurudi na manyoya machache kwani mengine yalisha peperushwa na upepo.

Kidele akamwambia " Fuledi mimi ni rahisi kukusamehe, lakini kumbuka yale maneno ni sawa na yale manyoya kuwa yalishapeperuka. Na wakati ukinyonyoa kuku alipiga kelele na watu wakakushuhudia. Na ulipoenda kuyafuata ukayakosa na wale watu pia walishaondoka, hivyo ni ngumu kuwatafuta na kukanusha kuwa hukuwa unayofoa yale manyoya"

Funzo

Ni kweli wengi wetu ni wepesi wa kuongea mambo ya uzushi hasa tunapohitilafiana bila kujua kuwa yale manano husambaa kwa haraka sana na huwakaa watu, pia huwa vigumu kuja kubatilisha usemi.

Hivyo basi ni vyema kuwa na busara kabla ya kutamka maneno yoyote dhidi ya wenzetu kwani maneno husafiri haraka

Unaposema huyu binti kicheche, Huyu jamaa mwizi mzushi na mengine kibao bila kuwa na uhakika jua kuna mtu anaumia kama ambavyo wewe ungeumia zaidi ukiambiwa

Jioni njema Marafiki

You Might Also Like

0 comments: