Mafanikio yaletwayo na matumizi sahihi ya FURSA
Siku moja Fuledi akasimama katika ngazi za kushuka kutoka katika sehemu moja maarufu na ambayo watu wengi walikuwa wakipita pale. Fuledi alishika fimbo yake na kofia mkononi na pia alikuwa amebeba bango kifuani mwake lililoandikwa kwa maneno makubwa " MIMI NI KIPOFU NAOMBA MSAADA"
Mtu mmoja msamaria akapita pale na kutoa sarafu chache na kisha kuziweka katika ile kofia. Kabla ya kuondoka akaligeuza lile bango na kisha kuandika maneno mengine ili watu wayasome na akaondoka zake.
Muda mfupi kila mtu aliyepita pale aliweka fedha nyingi kwenye ile kofia na yule kipofu akaanza kushangaa na baadae mchana ule yule mtu aliyebadilisha lile bango kwa maneno mapya akaja kuona maendeleo yakoje.
Fuledi akamtambua kupitia alivyokuwa akitembea na kumuuliza," wewe ni yule uliyebadilisha kibao changu?"
Uliandika nini?
Yule mtu akamjibu fuledi, "Niliandika yale yale maneno yako kwa namna tofauti" Mtu yule alikuwa ameandika: " LEO NI SIKU NZURI ILA SIWEZI KUIONA"
Je unadhani Fuledi na yule Mtu wote waliandika kibao chenye maana moja? Ni sahihi kuwa wote waliandika bango lenye maana moja kuwa Fuledi ni kipofu ingawa Fuledi yeye aliandika kuwa ni kipofu na alihitaji masada wa fedha.
Yule mtu yeye aliandika kuwambia watu kuwa wao walikuwa wakiifurahia siku kwa kuona uzuri wake lakini kipofu alishindwa kwa sababu haoini .
Je tunahitaji kushangaa kwanini maneno ya yulemtu yaliwagusa watu wengi na wakatoa fedha? Ni kweli yule mtu alitumia maneno yaliyomgusa kila aliyesoma bango lile na kuona anawiwa kutoa msaada au kushea furaha yake ya siku ile na kipofu yule
Hapa kuna mafunzo mawili ambayo twayapata:
1. Mshukuru Mungu kwa kile ulichonacho kwani pia kuna mtu/watu wanaweza tokea na kukupa msaada na kufanikisha matarajio yako.
2. Siku zote kuwa MBUNIFU, TUMIA FURSA ZILIZOPO MBELE YAKO na kumbuka SIKU ZOTE NJIA ZA MAFANIKIO HUWA USONI MWETU
0 comments: