Upendo wa mama haufananishwi na kitu

03:50:00 Unknown 0 Comments

Siku moja jioni mtoto fuledi alimfuata mama yake  jikoni akiwa ana andaa chakula cha jioni na kumpa mama yake kajikaratasi kadogo ambako fuledi alimwandikia


 Mama Fuledi alifuta mikono yake na kukichukua kile kikaratasi ambacho kilisomeka hivi:


Kwa ajili ya kukata nyasi nakudai : TZS  5000
Kwa kusafisha chumba changu wiki hii nakudai : TZS  4000
Unavyonituma dukani nakudai : TZS  1000
Kukaa na mototo ukiondoka : TZS  2000
Kutupa takataka nakudai : TZS  3000
Kusoma kwa bidii nakudai : TZS  5000
Kusafisha sehemu ya baba kupaki gari nakudai: TZS  1500
Jumla alidai: TZS  21,500

Mama akasimama pale baada ya kulisoma lile karatasi na baadae akatabasamu na kumpokonya peni na kuandika kitu kisha akampa fuledi asome.

Mama aliandika hivi:

Kwa miezi tisa niliyo kubeba  tumboni mwangu huku ukiendelea kukua:

Sitakudai

Kwa siku zote usiku ambazo sikulala kukubembeleza na kukupambia kitanda:

Sitakudai

Kwa miaka yote niliyokulea na ukanipa wakati mgumu na machozi juu yako:

Sitakudai

kwa nyakati zote za usiku ambazo sikulala nikikuuguza ili upone:

Sitakudai

kwa kila mdoli,  chakula, nguo na hata kelele zako:

Sitakudai

Mwanangu Fuledi, Hata ukiongeza upendo wangu kwako:

Sitakudai

Fuledi baada ya kumaliza kusoma huku macho yakijawa na machozi alisimama na kumwambia mama “Mama, Kutoka moyoni nakupenda.”  Na kisha akachukua lile karatasi na kuandika kwa kimombo “PAID IN FULL”.

Funzo:
·         Hutajua umuhimu wa wazazi  wako mpaka utakapo kuwa mzazi.
·         Uwe mtu wa kutoa kuliko kupokea kama wafanyavyo wazazi wetu
·         Kuna mengi wazazi wametupa zaidi ya fedha.
·          
BECAUSE  MONEY IS THE WORST WAYOF MEASURING HAPPINESS…

You Might Also Like

0 comments: