“AAAhhhhhhhhhhh!!! ”
Baba na mtoto wake walikuwa wakitembea
mlimani.Kwa bahati mbaya mtoto akajikwaa na kulia kwa sauti: “AAAhhhhhhhhhhh!!! ”
Mtoto alishangazwa kusikia upande wa pili sauti
ile ikisikika tena: “AAAhhhhhhhhhhh!!!! Akitaka kufahamu zaidi kwa udadisi
kasema kwa sauti: “Wewe ni nani ?” Sauti ikajibu tena: “Wewe ni nani ?” akiwa
na hasira kajibu kwa sauti: “Wewe muoga!” upande wa pili sauti ikajibu tena: “Wewe muoga!”
Mtoto akamwangalia baba yake na kumuuliza :“Baba mbona huyo mtu mkorofi na ananiigilizia?”
Baba akatabasamu
na kisha akajibu: “Mwanagu, Hebu sikiliza tena ” kisha baba akapiga kelel
akisema: “Nakukubali sana wewe!” Sauti toka pande wa pili ikajibu : “Nakukubali sana wewe”
Baba akaita
tena kwa sauti na kusema : “Wewe ni bingwa na jasiri sana!”. Sauti ikajibu tena
:
“Wewe ni bingwa na jasiri sana!”. Yule kijana alishangaa sana ingawa hakuelewa nini kinaendelea.
“Wewe ni bingwa na jasiri sana!”. Yule kijana alishangaa sana ingawa hakuelewa nini kinaendelea.
Kisha baba
akamfafanulia: “Mwanangu, watu sauti hiyo huiita MWANGWI, kwani huigiza sauti
na kuona kama mnabishana na mtu. Lakini MWANGWI huu tunaweza kufananisha na
maisha yetu,kwani kila baya au zuri ulisemalo hutokea. Maisha yetu humezwa na
matendo yetu tuyafanyayo,.
Mfano
Kama unahitaji
kupendwa na watu wengi hapa duniani, basi pia utatakiwa uandae nafasi ya upendo
katika moyo wako pia kwa watu wengine.
Kama unatamani
uwe na timu ya wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa kujituma,basi wewe uwe wa
kwanza kujituma kwa bidii.
Kama unapenda
kwa na marafiki wenye upendo na kukujali, basi wewe uwe wa kwanza kuwajali na
kwapenda
Na kanuni hii
ukiitumia katika kila kitu maishani mwako, basi utaishi kwa furaha na amani
kwani
Maisha ni sawa na mwangwi kila utakachokitoa basi tarudishiwa.
Maisha ni sawa na mwangwi kila utakachokitoa basi tarudishiwa.
Kama unataka mpenzi wako asikusaliti basi hakikisha wewe siku zote unakuwa mkweli kwake
0 comments: