... 'gramu 50!' ..... ' gramu 100!' .....'gramu 125' ...

09:10:00 Unknown 0 Comments

Profesa mmoja aliingia darasani na kuanza kufundisha akiwa ameinyanyua juu glasi yenye maji ndani yake.

Aliamua kuinyanyua juu ili kila mwanafunzi aione na akaanza kuuliza maswali kwa wanafunzi…..

"Niambieni, mnafikiri hii glasi ina uzito gani?"

... 'gramu 50!' ..... ' gramu 100!' .....'gramu 125' ...walijibu wanafunzi wale.

... "Siwezi kujua uzito wake mpaka niupime," alisema profesa, 

"Lakini swali langu ni hili hapa:

Nini kitatokea kama nitainyanyua glasi hii kwa dakika kadhaa?"

'hakuna kitu kitakachotokea' …..alijibu mmoja wa wanafunzi.

'haya sawa, na je nini kitatokea kama nikiendelea kuinyanyua glasi hii kwa saa zima?' aliuliza tena profesa.

'mkono wako utaanza kuumia’ alijibu mwanafunzi mwingine

"Uko sahihi sana, na je vipi nikiinyanyua kwa siku nzima?"

"mkono wako utaweza kufa ganzi kwa maumivu na wewe utashindwa kwani misuli ya mkono itashindwa kuhimili na nilazima utapelekwa hospitali kuuchua mkono!"

….. Wanafunzi wengine wakaanza kucheka baada ya mwanafunzi huyu kujibu majibu hayo

"Safi sana

Lakini je wakati wa haya yote yakiendelea uzito wa glasi ulibadilika?"

Aliuliza profesa.

'Hapana'…. Ndio jibu lililojibiwa na wanafunzi wote.

"Sasa ni nini kilichosababisha maumivu ya mkono na misuli kushindwa kuendelea kuishika glasi?"

Wanafunzi wakashindwa kujibu wakabaki wakishangaa.

"Nitafanyaje sasa ili mkono wangu upone maumivu?" aliuliza tena profesa.

"Ni kuweka glas chini tu!" walijibu wanafunzi

"Safi sana!" Profesa alijibu.

Matatizo katika Maisha hayatofautiani na mfano wa glasi hii.

Kuyaweka matatizo kichwani mwako kwa muda mchache huwa yanaonekana ni ya kawaida na hayana madhara kwako.

Unavyozidi kukaa nayo na kuyafikiria kwa muda mrefu nayo huanza kukuumiza

Ukikaa nayo muda mrefu zaidi nayo hukuzidi na hutaweza kufanya lolote kuyazuia tena.

Ni vyema kwetusote kujua kuwa matatizo katika maisha yapo na jambo la msingi ni kuyamaliza yakiwa bado chiniya uwezo wetu na kabla ya kuzua madhara ambayo kuyazima huwa sio kazi rahisi.

Lakini kitu cha msingi kabisa ni kuhakikisha kila siku unaporudi kulala unakuwa umeyatatua matatizo ya siku hiyo na kuhakikisha unalala ukiwa na amani ya kutosha huku ukipa nafqasi akili yako kufikiri mambo mapya.

Na ndio maana utaamka ukiwa huna msongamano wa mawazo (stress), ukiwa huru na mwenye nguvu za kuhimili mikiki mikiki ya siku mpya. Na kila jaribu litakalo kufikia unakuwa uko tayari kulitatua.

Nakutakia siku njema na nina imani utakabiliana vyema na siku ya leo na iwe yenye neema.!

Napita tu hapa

You Might Also Like

0 comments: