Mwaka 2016 utakufa kwa ukimwi kutokana na tabia ya kupenda vibinti

15:39:00 Unknown 0 Comments

Jamaa kaenda kwa mganga na kumwomba amtabirie maisha yake

Jamaa: mganga naomba unitabirie maisha yangu 

Mganga: Sawa sawa kijana wewe unafanya biaasha ya kuuza karanga sio?

Jamaa: Tawire mganga

Mganga: Basi biaashara yako itakua sana na utaanza kununua magunia ya karanga na kwenda kuuza kariakoo

Jamaa: Asante baba mganga

Mganga: Utapata umaarufu hapa kijini na na hata Tz nzima itakufahamu na utakuwa unatoa udhamini kwenye events kubwa kubwa na kuheshimika

Jamaa: Hapo mganga umesema na wewe nitakupa hela kibao sana sana

Mganga: Wawekezaji wengi ndani na nje watataka kuwekeza kwako kutokana na kampuni yako kukua na utapata kufahamika kimataifa nakuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama bilionea

Jamaa: Mganga kweli hapo lazima nikupe hisa na fedha kibao... ongea onge mganga wangu wa nguvu

Mganga: Mwaka 2016 utakufa kwa ukimwi kutokana na tabia ya kupenda vibinti

Jamaa: Acha umbulula wewe mganga gani...ebo (huku akitimua mbio)

You Might Also Like

0 comments: