Siku nne baadae akaanza kuhisi maumivu makali

00:59:00 Unknown 0 Comments

Jamaa katika Maisha yake hakuamini hata siku kama ingekuja kutokea yeye na mpenzi wake wakasalitiana.Hakuamini hasa ukizingatia malengo waliojiwekea na jinsi walivyotoka mbali kwa pamoja wakipeana ahadi za kuja kukaa wote.

Jumatano ile akiwa na uchovu wa kazi na anajiandaa kutoka kazini alipokea ujumbe kupitia facebook kutoka kwa rafiki yake kuwa mpenzi wake yupo na jibaba moja wakila yao ndani ya hoteli moja maarufu na kwa bahati nzuri akiwa anajiandaa kukurupuka anapokea na picha ya wawili hao wakiwa wanaingia hotelini.

Kwa haraka aliondoka na kwenda hotelini pale na kuwakuta wawili wale wakiwa wanakula raha pembezoni mwa swimming pool.Baada ya kuona wote wamemwona aliamua kuondoka na kwenda bar moja na kuanza kujitwika pombe zisizo na break.

Akiwa pale bar kalewa chakarii akamchukua binti mmoja aitwaye na kuamua kwenda naye hotel kwani asingeweza rudi kwake ni usiku na hasa ukizingatia alikuwa kalewa vibaya.

Maumivu ya kichwa ndio yaliyokuja kumwamsha saa tisa mchana siku ya pili yake,na maumivu yale yaliashiria pombe nyingi alizotwikwa jana yake.

Bado akawa hajui wapi alipo na upande wa pili kalala binti ambaye baada ya kumwamsha akamsimulia jana yake alivyomsaidia afike pale kwani alilewa sana na alikuwa hajitambui.

Jmaaa kucheki mida ni saa tisa na alitakiwa saa moja awe ofisini kwake na ni operator wa zamu katika kampuni ya ujenzi na hana cha simu wala hela mfukoni ikambidi amwombe yule dada ampe 5000 ili aitumie kufungua laini yake awasiliane na jamaa zake na nauli ya kwenda home.

Majuto

~Akaifungua line yake akitegemea salio lake toka M-PESA lakini akagundua ya kuwa fedha zote zilitumia usiku wa jana na yeye huweka fedha nyingi kwenye mtandao wa simu zaidi ya benki kwa hiyo akaanza kuumiza kichwa alizitumiaje fedha zile

~Siku ya pili akaenda kazini na kukuta barua ya kusimamishwa kwani hakutoa taarifa na aliingizia kampuni yake hasara kubwa katika kazi ile ambayo yeye kama msimamizi alitakiwa awepo au simu iwe hewani kama ana dharula.

~Siku nne baadae akaanza kuhisi maumivu makali wakati akijisaidia haja ndogo na alipokwenda kuchekiwa hopst wakagundua ni gono ikambidi aanze tiba.

~Baada ya kupona gono na kuanza kusahau yale maumivu na akiwa bado anaendelea kuhangaika ili aipate kazi mpya, yule binti akampigia na kumwambia ana ujauzito wake, kwani yeye alikuwa mbishi kutumia condom na yule dada alimwambia kuwa alikuwa siku mbaya ambazo angeweza kushika mimba…. Hivyo ikawa hana jinsi zaidi ya kukubalina na janga hili jipya.

Funzo

Msongamano wa mawazo ni jambo ambalo ni gumu kwetu sisi sote kukabiliana nalo,na ukishindwa kujizuia madhara yake huwa makubwa na yenye maumivu na majuto makubwa kwa Maisha yako, uhusiano wako baina na Mungu wako na pia watu uwazungukao.

Hebu angalia mfano wa jamaa kumfumania mpenzi wake imemsababishia kupoteza fedha, kupata gono, kufukuzwa kazi na sasa ni baba mtarajiwa. Je mtoto huyu amwite majuto? Je atampenda kwa dhati mtoto huyu na mama yake?

Je haikuwa njia ya MUNGU kumwonyesha jamaa kuwa mpenzi wake sio mkweli labda sasa anatakiwa akae naechini kumwonya au aangalie ustaarabu mwingine?

Kila jaribu huwa na maana yake na ni vyema kuwa mpole kuituliza akili na kuangalia kipi cha kufanya kwa usahihi na busara.

You Might Also Like

0 comments: