Ujumbe kwa Baba na Mama

11:11:00 Unknown 0 Comments

Ujumbe kwa Baba na Mama 

Mama sikukuchagulia baba... Ila wewe ulimchagua... Baba sikukuchagulia mama ila ni wewe uliyemchagua na kuanzia hapo mambo yakaanza kusonga name nikatokea…….. 

Niangalie sasa mimi, nimekuwa kijana mkubwa na nina jitegemea sasa, Nisingeweza kuwa hapa nilipo bila nyinyi, Bado nahitaji uwepo wenu katika safari yangu ya maisha hapa duniani... 

Na kama nikipata matatizo kazini hata sehemu yoyote ile nyie wazazi wangu ndio huwa kimbilio langu.... Nahitaji kuwaombea kila siku ili mzidi kuishi na kushuhudia mafanikio yangu na mfurahie kuwa na kijana kama mimi……

Nitamwomba mwenyezi MUNGU anipe hekima na utii wa kuwafanya mfurahi kila siku yenu ya Maisha hapa duniani kama nyinyi mlivyonipa furaha isiyo na kipimo tangu ningali mdogo mpaka leo hii….

Pia bado nitahitaji mnifundishe jinsi ya kuwapa furaha ile mtakayo nami nitafanya hivyo kwa mapendo ya dhati kwenu wazazi wangu wapendwa….

Nitawakumbuka sana kipindi ambapo hamta kuwa nami tena hapa duniani hivyo huu ni wakati wangu wa kuonyesha upendo wangu wa dhati kwenu…

Nawatakia siku njema Baba na Mama.... 

You Might Also Like

0 comments: