tukiwafanyia umafia mnadai sisi sio lakini haya mambo yanaumiza sana.

14:57:00 Unknown 0 Comments

Jamani mbona kuna wanaume hawana huruma kwetu sisi kina dada wanaodhani maisha yametukwepa?????

Mimi ni dada ambaye ninafanya kazi ya kuuza vinywaji na chakula katika bar moja maarufu hapa jijini.

Amekuja mtu anadai dada tafadhali nipo na familia yangu na ningeomba tupate mahitaji, mie kiroho saafi namhudumia na baada ya huduma wamekula na kunywa bili inafikia laki na kitu.

Nampa bili anadai naomba nikulipe kwa mpesa,mimi nakubali kwani haina madhara akanirushia na ya kutolea.

Inafika muda niende kutoa na wao walishaondoka saa nyingi, naona salio halitoshi na wakati alinitumia,nimewapigia voda wanadai yulemtu baada ya kutuma aliwapigia na kudai alikosea namba alikuw akituma sehemu nyingine na sio kwangu.......

Yaaani laki na kitu mimi nitaipata wapina kuirudisha kazini?????

Watu tukiwafanyia umafia mnadai sisi sio lakini haya mambo yanaumiza sana.

Hebu fikiri natembea usiku katika hatarishi,siwezi sema tumebakwa mara ngapi tukitoka katika kazi hizi ili na sisi wanetu wafurahi kama yeye lakini hapa mie naonekana mnyonge.

Nimeumia sana marafiki naombeni ushauri wenu

You Might Also Like

0 comments: