Ujumbe wa kwenye khanga wazua majanga

20:57:00 Unknown 0 Comments


Jamaa kagombana na mkewe, Kasusa kula, kurudi kazini kamkuta mkewe
kavaa kanga imeandikwa "Ukisusa wenzio wala" ilipofika usiku mke kachukua karata aina ya "mzungu wa n4 akaiweka kitandani katikati" ilipofika asubui mke kavaa kanga
imeandikwa "ukitoka mwenzio anaingia"

Jamaa akagoma kwenda kazini. Mke akavaa kanga imeandikwa "Hamniwezi nimemdhibiti ndio maana hatoki" Jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akamwambia twende
nyumbani.

Walipofika nyumbani wamemkuta mke kavaa kanga imeandikwa "ulidhani rafiki yako
kumbe adui yako" Kwa kumalizia mke akasema "shemeji utaendelea kula kaka yako kasusa"

Mpaka muda huu jamaa yupo ICU

You Might Also Like

0 comments: