HEBU TUONGELEE COPY AND PASTE

19:14:00 Unknown 0 Comments




Kwa uzoefu mdogo niliupata kutokana na media tukihusisha na kazi mbalimbali tuzifanyazo.

Kumeibuka wimbi zuri sana la kupashana habari kwa mtu kuchukua habari kutoka chanzo kimoja na kujimilikisha habari ili aweze kuwapa habari hiyo wengine ( Copy & Paste )

Kama wewe huna page na plan yako ni kuhabarisha tu, haina shida saana ila unatakiwa uelewe kuna umuhimu wa kukielezea chanzo cha habari hiyo maana kama ni ya uzushi basi na wewe huonekana ni mchapichaji lakini kama ungeweka chanzo basi wewe huwa na nafuu.

Kama wewe una page, blog au una tumia akaunti yako kwa kazi mbalimbali ikiwepo za ubunifu ukiweka mambo uyafanyayo ili kuhabarisha watu basi epuka copy n paste.

Kwani nini nasema hivyo.

kwa muda mfupi unaweza onekana kuwa wewe ni bingwa wa kuandaa makala hizo kabla ya watu kuja kumjua mhusikana na nikuanzia hapo hutaandika kitu watu wakaamini ni wewe na kukosa mashabiki.

Kitu kingine ni sawa na mimi leo kuanza kazi ya utangazaji na kuamua kuiiga sauti ya ndugu na mdogo wangu King Dav au nikaanza kuimba na kuiiga sauti ya Mary Lucos bila kujua ninachofanya ni kumpa umaarufu yeye zaidi kwani watu wengi wanamjua hivyo itakuwa ngumu kwangu kuwafanya mashabiki watofautishe..... Hapa cha msingi ni kuafuata nyayo za King David na Mary Lucos na mwishoe mie kuwa na style yangu wao nikiwatumia kama role model wangu.

Kitu cha muhimu zaidi copy and paste huaribu uwezo wa mtu kufikiri kwani kuna kipindi huwezi fikiri tena na kujiona ukiozidi kudorora na kushindwa kuhimili ushindani tena.

Na kama unatumia copy and paste ili kupata watembeleaji wengi katika site yako jua utapata wakati mgumu sana kuweza kudumu na hali hiyo kwani watu huamia kwa wanayedhani hafanyi hivyo.

Kitu cha msingi kuwa na ladha tofauti ya kuwa na watu tofauti na itakujiengea jina na mapokeo tofauti.. Huwezi kamwe kuwa kama Morgan Mokili-mobimba Baba-wizle au Fadhy Mtanga kwa kuiga kila akifanyacho.

Lakini waweza kuwa na utofauti mzuri na mapokeo mazuri katika kazi zako kwa kujifunza nini anakifanya Breaking Newz ili nawe uje na maboresho mazuri kwa kazi zako na sio kuwa na kila kitu afanyacho yeye.

kama dunia nzima tungeamua kuiga utengenezaji wa gari aina ya Land Rover basi kamwe watu wasingefikiri kuna uwezo wa kuwa na gari aina ya Mercedes-Benz

Au kama wote wangetangaza kama Grace Kihampa unadhani tungeweza kuwa na vipindi vingine????

Hebu fikiri kama nami leo nipost habari zile ambazo Seth De Jesus Giovanni anaziweza unafikiri nitaweza?

Kila kitu ukifanyacho ni brand ya wewe hivyo jaribu kuwa tofauti kama jina lako lililovyo

Samahani kama inakuhusu sina maana mbaya ni mtazamo tu tusijenge chuki


Nipe maoni yako juu ya Copy & Paste kwa kubofya HAPA

You Might Also Like

0 comments: