kwa wenye mazoea ya kutopokea simu tuu ndio wasome hapa
Mkewe alikuwa hoi akisumbuliwa na homa za mara kwa mara zilizotokana na ujauzito aliokuwa nao kabla ya mauti yake kumkumba.
Kwa kuwa chumba kilikuwa kina baridi na hasa ukizingatia mkoa aliokuwa akiishi ulikuwa na baridi basi mke alichukua jiko la mkaa na kuwasha moto na kisha kuuingiza ndani ili apate joto.
Mkaa ule kwa kuwa haukuwa umekolea vyema ukaanza kufanya hewa yamle ndani kuwa ya shida na mke akachukua simu na kumpigia mmewe lakini hakuwa na tabia ya kupokea simu akipuuzia na kuendelea kunywa pombe na mabinti zake.
Masaa manne baadae kijana alirudi na kushuhudia mkewe akiwa amekauka kwa sumu ya mkaa, kijana alianza kulia kwa uchungu akijutia kuidharau simu ile lakini hakuna lililofanyika zaidi ya kuendelea kujutia.
Maisha yake yakabadilika na kuwa ya shida na akawa kama ana mikosi katika maisha yake na kila siku akimwomba Mungu amsamehe kwa kosa lile. Na sasa hakuwa na msaada tena kwani marehemu mke wake ndiye alikuwa akifanya kazi na kuleta kipato cha familia.
Kijana yule akawa akicheza bahati na sibu mbali mbali huku akimwomba Mungu amfanye apate fedha naye atahakikisha anafanya mambo makubwa kwa jamii yake.
Baada ya miezi mingi kupita siku moja jioni majira ya saa moja alikuwa sehemu akinywa pombe na baadhi ya marafiki zake, simu yake ya mkononi ikaatia namba ngeni zaidi ya mara nne na wenzake wakamshauri apokee ile simu lakini kama kawaida ya dharau zake akaipuuzia na kuendelea kunywa.
Siku ya pili asubuhi akiwa na uchovu na akijifikiria jinsi ya kulipa kodi ya nyumba akiwa hana hili wala lile akaona ngoja aingalie upya ile namba iliyimpigia zaidi ya mara nne.Akaichukua simu na kuipiga na muda huo ilikuwa tayari ni saa za kazi.
Baada ya kuongea na kuikata simu ile kijana alipiga kelele zenye vilio vya ajabu akisema ana mkosi gani? Kwani simu ile iliyopigwa zaidi ya mara nne jana yake usiku ilikuwa ni kutoka katika kampuni moja kubwa ya simu nchini na kijana alikuwa akipigiwa kuambiwa kashinda bahati na simu ya shilingi milioni 200.
Na kwa kawaida ya kampuni ile baada ya namba kujitokeza ya mshindi hupiga simu mara tatu tuu na asipopokea huchaguliwa namba nyingine, lakini kwake walipiga na moja ya ziada na kuwa mara nne lakini simu haikupokelewa…… Hivyo bahati ikatoweka kwa uzembe wa kutopokea simu
Mara ya kwanza alimuua mkewe kwa kutopokea simu na sasa utajiri umemkimbia kwa kutopokea simu


0 comments: