Wakati wewe una inyanyasa familia yako leo, kumbuka kuna mtu anatamani apewe familia na aipende

16:00:00 Unknown 0 Comments



Mzee akilia kwa uchungu baada ya kuokota albamu yenye picha za kumbukumbu za familia yake ambayo imekubwa na tetemeko na wote kufariki na kumwacha yeye mwenyewe.

Wakati wewe unaidharau familia yako na kuikimbia ukiitelekeza kuna watu wanalia kupata watu wa kuwafariji

Wakati wewe unatoa mimba, kuna mtu anasaka mimba kwa miaka kumi bila mafanikio

Wakati wewe unaiharibu amani ya nyumba yako kumbuka kuna watu wanajaribu hata kutumia hela kupata amani na wanakosa

Wakati wewe kijana una mkataa binti uliyempa mimba, kuna mzee ana miaka nenda rudi akiwa anakesha akiomba Mungu amjalie mtoto

Wakati wewe una inyanyasa familia yako leo, kumbuka kuna mtu anatamani apewe familia na aipende

Wakati wewe unaichukia kazi uliyonayo, kuna mtu ana vyeti vyake safi ila hajawahi kupata kazi ya aina yoyoye na anaishia kwenye interview tuu

Wakati wewe unawadharau na kuwasahau wazazi wako bila kuwajali. Kuna watu wanalia usiku kucha na kuumia kuwakosa wazazi

Una kila sababu ya kuwa na amani na kuipenda familia yako sasa kabla ya kuja siku ambayo utaumia kwa kutowafanyia mema na wakati huo hautakuwa nao tena.

Pia kumbuka, hakuna maisha yoyote zaidi ya haya na huna budi kuwa na shukrani kwa kile unachojaliwa sasa.... Pia ni bora kuwa na mpangilio wa maisha ukimtanguliza MUNGU na kushukuru kila ulichonacho na kufurahia nyakati ulizonazo.

Comment Naipenda familia yangu na kisha share

Niunge mkono kwa ku-like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: