Ama kweli mjini akili nguvu huko chimala...... Kiserengeti boy chamliza mama fedha ya ada za watoto na marejesho ya mkopo kisa neno "baby"
Jumamosi moja majira ya saa saba tulikuwa tumekaa maeneo ya kujivinjari nje ya bar moja yenye vyumba vya kupangisha pia.
Tukiwa tunaendelea kupata moja moto moja baridi huku maongezi yakiendelea mara kuna gari moja dogo likasimama na mara akashuka kijana mmoja akiwa na mama mmoja ambaye alionekana kuwa wa makamo kiasi.
Wakawa wanasaidia kufunga milango la gari na kushikana mikono wakiitana baby na kama haitoshi kiss moto moto zikiendelea kwa mwendo wa halaiki.
Kweli nikasema serengeti boy amepata zali na mama anaufurahia uzee wake kukamilifu kwa kuitumia rasilimali hiyo.
Kwa jinsi walivyoonyesha kupendana na kufurahi kwa pamoja ni kama wana miaka zaidi ya minne ya mahusiano hayo.
Baada ya kupata bia moja mbili wakaomba chumba kwa mhudumu na kuzama ndani na sio kutuacha tukijadili juu ya wawili hao.
Mazungumzo na vinywaji viliendelea huku tukilijadili sana suala la vijana kujilipua aka kujitoa mhanga kiasi cha kuvamia majimaa.
Wengi tulisema ni ugumu wa maisha na kuwa vijana wengi wa mjini hawapendi kazi na kutafuta miteremko.
Tukiwa katikati ya mada na ni zaidi ya saa tangu kijana yule wa kujitoa mhanga kuingia mle ndani akiwa na number one wake mshuhudia akitoka na begi na kuingia kwenye gari lake na kuondoka akiwa mwenyewe.
Mmmmmmh tukasema kwa pamoja lazima kijana katumwa ATM akadake fedha au anafuata mambo mazuri amletee mkewe aka jimama.
Haikupita dakika kumi yule mama alitoka ndani akiwa mbio tena na nguo alizozaliwa nazo akipiga kelele nimeibiwaaaaa!!!!!!!!!!!!!
Ikabidi dada wa guest ile ampe kanga ajisitiri maana ikulu ilikuwa wazi na ni hatari kwani angeweza kushambuliwa na wanamgambo wa Alshababu ikawa balaaa.
Baada ya dakika mbili tatu za kumtuliza hatimaye tukaupata mchapo mzima kuwa yeye ni mke wa mtu na huyo baby walikutana njiani na akampa lift na kuonyesha ana utaalamu wa maneno yenye sukari ambayo mama hakuwahi kuyapata.
Na wakati huo mama ametoka kwenye taasisi fulani alikotumwa na mmewe ambaye ni mgonjwa kuwa akachukue mkopo wa milioni nane kwa ajili ya matibabu ya baba, matumizi, ada za watoto wasomao intaneshno school na pia kuongeza mtaji wa biashara ya mama.
Na baada ya kumaliza mambo yao mle room kijana akaingia kuoga na baada ya kuoga akamwomba na jimama akaoge na kuutumia mwanya huo kukusanya fedha mpaka nguo za ndani za jimama na kisha kusepa nazo.
Mimi sikuwa na ushauri ingawa rafiki yangu msugaule na nyaulingo wakasema mama atafute nyembe ajichane mwili mzima na kugalagala kwenye tope akadai kwa mmewe kuwa ameporwa na vibaka ili aokoe familia.
Mama alilia kwa na hakukuwa na msaada wowote.
Mpaka leo nikikumbuka maneno ya baby nahisi kuna mtu ataibiwa.
Amakweli mjini akili nguvu huko chimala
0 comments: