Binti yetu wa kazi alikuwa jini na tuliishi nae bila kujua

10:02:00 Unknown 0 Comments



Baada ya kukaa na binti wetu wa kwanza aliyekuwa akituhudumia kama msichana wa ndani kwa muda mrefu, mimi na mme wangu tukaamua kumpeleka shule ya bweni ya ufundi kama shukrani ya kuwa msaada kwetu kwa muda mrefu.

Wakati dada yetu kaondoka kuna dada mmoja tulifanikiwa kumpata kutoka kijijini na akanza kutusaidia kazi tukimwachia watoto wetu wawili ambao walikuwa bado wadogo akawa akiwaangalia tukiwa kazini.

Kwa mara ya kwanza nikaanza kugombana na mme wangu bila sababu ya msingi. 

Kila tukijaribu kukaaa wala hatufikii muafaka zaidi ya kufarakana na nikaanza kuichukia familia yangu bila hoja ya msingi.

Nakumbuka kuna siku nikafungasha vitu nirudi kwetu kabla ya mama yangu wa hiari pale mtaani kunisihi niache upuuzi huo na kuamua kubaki huku nikiwa sitaki hata kuung'aza uso wa mme wangu na wanangu pia.

Vioja vikazidi kila siku nikirudi nyumbani watoto wananiomba wacheze na nyoka nami nikiaanza kuona kama nyumba imeingiliwa na wakati nikifikiri hilo nikaanza kuona mara tuokote fedha mlangoni na hatujui nani kaziweka.

Nawaambia watoto wasizichukue na kumwambia mme wangu akawa anazitupa nje mbali na tukiamka asubuhi tunazikuta ziko mlangoni na ni nyingi zaidi, kazi ikawa ni ya kuzitupa tu kila siku na kurudi tena na hakuna aliyezichukua.

Mmmh nyumba ikaanza kuwa sio nyumba mara ng'ombe wetu wawili wakafa na kuku wakaanza kufa ovyo ovyo bila ya kujua ni nini kinachosababisha.

Ilinibidi nimwombe mme wangu kukae na kuanza kusali kwa pamoja. Jioni ile yule dada wa kazi wakati tunasali aliondoka kwenda jikoni na tukashangaa.

Siku ya pili asubuhi nikiwa ofisini nikapigiwa simu na namba ya ajabu na baada ya kuipokea mtu ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake akaaniambia, tuache  kumshirikisha dada yetu katika sala na kuwa tukikaidi na kuendelea na akafa basi moto utatuwakia.

Niliogopa sana na kumpigia mme wangu na akaniambia kapigiwa pia na namba ya ajabu na imejifuta pia.

Jioni tukakutana na kwenda kwa mchungaji na baada ya kumwambia kwa kina tukamchukua mpaka nyumbani.

Kufika pale na kuanza sala lakini kila tulipozidi kusali dada alizidi kujikuna mwili mzima huku akishindwa kuhema na kuanza kusema nisameheni mimi nilitumwa kuja kuwaharibia furaha hapa kwenu.

Akaendelea kusema na kila watoto waliposema wanataka kucheza na nyoka ni mimi nilikuwa najigeuza na kuwa nyoka na kuanza kucheza nao nyie mkiwa kazini.

Wakati wote tumeduwaa akatuambia na ile mifugo yetu liyokuwa ikiumwa, kufa na hata watoto kuumwa alikuwa ni yeye na zile hela kama tungeokota na kuzitumia tungekufa.

Siku ya pili tulimrudisha kijijini ambako baada ya kupokelewa muda mchache tukiwa njiani tunarudi tukapigiwa simu kuwa katoweka.

Basi tukafika nyumbani na kuendelea kuomba na zile fedha zilianguka kwa siku kadhaa na kisha zikatoweka na furaha yetu ikarudi mara mia ya ile ya mwazo na nikamshukuru Mungu kwa hilo.

Miezi michache baadae nikiwa kazini nachezea simu yangu nikaiona namba ya yule mtu aliyenipigia na kunionya na nikaipiga ile namba na kujifanya nipo Dar, alivyopokea nikajifanya wrong number.

Jioni narudi nyumbani mme wangu akaniambia kuwa leo nilipiga simu wapi? Baada ya kumdanganya kuwa sikupiga simu yoyote akanionyesha ile ile namba na kuniambia wamempigia wamedai nisiwafuatilie.

Mmmh nikaogopa na kuendelea na maombi na mpaka sasa maisha yetu ni yafuraha na sitaki tena wasidizi wa ndani ya nyumba...........

Hadithi hii ni ya kutunga haina ukweli wowote......

Ila share

You Might Also Like

0 comments: