Stress zilitaka kunitoa roho yangu ( kisa cha kweli)

10:05:00 Unknown 0 Comments


Mwalimu wetu chuoni aitwaye Mr Stan aliingia darasani siku hiyo na kutufundisha kuwa msono wa mawazo (stress) ni ugonjwa hatari sana kwa binadamu yeyote yule.

Na ugonjwa huu kama binadamu usipokuwa makini na kujifunza namna ya kuzuia au kukosa wa kukupa nguvu basi unaweza ukafa, kukonda na hata ukaona huna maana ya kuishi tena.

Nakumbuka kulizuka mjadala ulioongozwa na mimi na nilimbishia sana na kumwambia kuwa huko ni kujiendekeza kwa mtu na kuwa sio mvumulivu wa kutatua masuala yake.

Mwalimu hakuongeza neno na kusema tuiache topic hiyo kwa muda na kila mtu afanye utafiti mtaani, majumbani na kujifunza na kuna siku kabla ya semista kuisha atatuuliza na kila mtu akaendelea na utafiti huo na maisha ya chuo yakiendelea.

Siku moja nikiwa nimetoka mtaani nilikopanga naelekea chuo njiani nikapokea ujumbe kutoka namba ngeni kuwa nimebandikwa katika ubao wa matangazo nahitajika ofisi ya utawala.

Nikafika pale nikiwa nina maswali nahitajika kufanya nini.

Nikapewa barua iliyonionyesha kuwa niliandaa party ya kidarasa kinyume na taratibu za chuo hivyo natakiwa nisimamishwe masomo na kama haitoshi mahudhurio yangu chuoni yana walakini hivyo nimepoteza sifa za chuo.

Mikono ikaanza kutoka jasho na wakati huo nikajaribu kujitetea juu party hiyo kuwa ni darasa tulipanga na sio mimi peke yangu.

Nilipoona sisikilizwi nikaomba kwenda kwa mwalimu wa darasa ambaye alinikana katakata na kusema yeye hausiki na alinikataza juu ya party hiyo.

Kichwa kikaanza kuuma na sikuwa na cha kufanya ikanibidi niende serikali ya wanafunzi ili rais wa chuo anisaidie kwani naye alialikwa kama mgeni rasmi siku hiyo.

Rais alikataa kuongea nami na kuniambia, "Fuledi usitake kunipekeka polisi na mimi kwa party uliyoiandaa kinyemela na kusababisha mauaji huko"

Nikauliza mauaji gani rais???????

Akasema kati ya wale vijana wa mtaani waliokuwa wakigombana pale mmoja kafa na nafikiri polisi wanakusaka sasa.....

Kweli nikakumbuka kuna ugomvi wa vijana wawili wa pale mtaani walivamia party na baade waligombana ila nikajiuliza ugomvi ule una mahusiano gani na party?

Muda huo wanafunzi wenzangu walishatawanyika na kila niliyempigia simu hakupokea na kumpata mkuu wa chuo muda ulikuwa umekwenda.

Nikajivuta mpaka kituoni ila nguvu ya kupanda daladala ikawa imeniishia, nikachukua tax mpaka nyumbani na kujilaza kitandani huku nikiwaza naota au ni kweli hayo yametokea?????

Na je naachishwa chuo mkopo nitalipaje au nitapataje ili niende chuo kingine? Nyumbani nitawaambiaje na hasa nikifikiria maisha ya kwetu na mama na baba walivyonitegemea nipate hela ya field tugawane????

Niliishia kulala bila hata ya kula mpaka siku ya pili na kudamka saa tano nikiwa nimechoka na mwili hauna nguvu.

Sikuwa na cha kufikiria muda huo zaidi ya kwenda kununua sigara na pombe kali kwani kuna rafiki yangu alishawahi niambia huwa za mpunguzia mawazo lakini baada ya kuzinunua na kabla ya kunywa wazo likaja na kusema fuledi acha ujinga nenda chuoni kaonane na mkuu wa chuo.

Nikafika pale chuoni na kila mtu alionekana kunishangaa bila kusema chochote nikagundua kuwa sikuwa na furaha ya kawaida nikaenda kwa mkuu wa chuo naye hakusema jipya zaidi ya kusema fuledi mimi sitaweza kukusaidia zaidi ya kufuata taarifa za kina nilizozipokea juu yako.

Nikaondoka pale na kuamua kwenda darasani na kufika mlangoni nikaona mwalimu Stan akiwa na wanafunzi pale nje na hakuna aliyeonyesha kunichangamkia na baadhi nilivyokuwa nikijaribu kuongea nao juu ya party kila mtu alinikwepa kama mwenye ukoma hata rafiki zangu wa karibu.

Jambo lililonikatisha tamaa ni kwamba hata mwalimu stan ambaye ni rafiki na mwalimu na kwenye party alialikwa pia akatamka kuwa fuledi kwa nini uliandaa party ya kutuchafua???

Sikuongea neno na kuondoka zangu kwenda nyumbani na barua ya kuachishwa chuo sikwenda tena kuichukua.

Nilifikia bar na kuanza kunywa na hapo mwanzo sikuwa mnywaji, nakumbuka kwa wiki ile nilianza kujiona naisha, sina hamu ya kula zaidi ya pombe, sina uelekeo na mbaya zaidi nina mawazo na hasira kila mara.

Nakumbuka ilikuwa jumapili saa nne usiku alinipigia mwalimu stan na kusema nahitajika jumatatu saa mbili asubuhi kwenye kipindi chake kwani kuna jambo la msingi sana.

Nilikata simu na kuizima na kusema kamwe siendi ila kuna kitu moyoni kikaniambia nenda yawezekana wameniombea msamaha.

Nilipofika darasani mwalimu alisema karibu fuledi pita mbele.... Nikaenda kunyonge na baada ya kufika pale akasema waambie darasa ....... Stress zina madhara gani??????

Kwa ufupi nikasema stress ni kaburi lako..........

Darasa zima walicheka na ndipo mwalimu akasema hata chuo hukufukuzwa ila tulitaka kukamilisha kazi hii kwa vitendo kuhusu somo la msongamano wa mawazo (stress) na athari zake

Amini usiamini kwa siku chache nilizokaa na mawazo yale nilihisi kaburi langu lipo hatua chache toka kwangu.

Epuka stress ishi kwa furaha sasa

Kama umeelewa share habari hii na niambie mtazamo wako juu ya ugonjwa huu kupitia comment

Whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: