Fedha za kuokota barabarani kidogo zimtoe uhai juma... Mwili wavimba kama kaungua

17:19:00 Unknown 0 Comments



Juma aliamka asubuhi na mapema na kujiandaa kuelekea kwenye mihangaiko ya siku hiyo akiwa hana hata senti moja mfukoni mwake.

Akaagana na mkewe kipenzi na akakatiza njia ya mkato ili awahi kufika kijiweni kwake na kuona siku hiyo kuna neema gani mbele yake.

Katika uchochoro mmoja kwa mbali akaona bahasha ambayo baada ya kuisogelea ndani yake kukawa na hela nyingi sana.

Kwa kuwa hakuwa na fedha akazichukua na mbio akakimbi na kwenda wakala na kuzirusha kiasi kwenye akaunti yake na kiasi akaacha na kununua baadhi ya mahitaji na jioni akarudi nyumbani na kuhifadhi baadhi ya fedha zile.

Muda mchache baada ya kula chakula cha jioni juma akaanza kuhisi joto linapanda mwili mwake na akaomba apewe dawa na kwenda kupumzika.

Usiku ule joto lilizidi naye akajikaza kiume na asubihi akawahi kwenda kuchekiwa na hakuonekana na tatizo lolote zaidi ya kupewa dawa za kupunguza maumivu na kuambiwa apate muda wa kupumzika.

Mpaka kufika jioni ya siku hiyo mwili wa juma ukawa na malenge lenge ya maji kama mtu aluyeungua na moto vile huku akilia kwa maumivu.

Mkewe hakujua nini cha kufanya na kumuuliza labda kuna kitu kakifanya au zile hela aliiba sasa amewekewa madawa lakini bado juma alisisitiza kuwa hakuiba hela wala hana ugomvi na mtu.

Hali ikazidi kuwa mbaya na wakati huu mwili wa juma ukawa kama kidonda kwani yale malenge lenge yakawa yakitoboka na mwili ukitoa harufu mbaya na kunata kwenye nguo na mashuka.

Ndugu na jamaa wakakusanyika siku ya nne kwani sasa hata hospitali wakawa kila wanachokijaribu hakileti matunda na kushauriwa kukaa kifamilia na kujadili nini cha kufanya kwani juma asingepona.

Wakati wote huo mke wa juma hakuisha kulia na kwa kushirikiana na mama yake juma wakaamua waende kwenye nyumba ya ibada.

 Baada ya kuombewa maajabu ni kwamba mwili wake ulitokwa na vitu vya ajabu vikiwa vinaongea kuwa viliwekwa kwenye hela ila mtu atakaye okota afe na aliyezitupa zile hela apate utajiri.

Juma kapona na mpaka sasa karudi hali yake ya mwanzo na kila akikumbuka kisa kile kamwe haishi kumshukuru Mungu kwa kumnusuru uhai wake katika kifo cha kishetani.

Ndugu yangu kamwe usijaribu kuokota kitu usichokijua kwani huwezi jua kimewekwa hapo kwa namna gani na pia huwezi jua aliyekiweka alinuia nini au hata aliyekipoteza alikitumia na kukipa ulinzi wa namna gani.

Mungu awe mlinzi wetu kwani twapokea vingi vinavyotoka kusikofahamika hivyo ni Mungu pekee wa kutuepusha na haya.

Comment Amen kuonyesha ni Mungu pekee mwenye uweza wa kutulinda na kutuepusha na hila za ibilisi shetani na pia share kuonyesha nawe unawajali ndugu zako na wapenda nao wahabarike na kuwa makini.

Like ukurasa wetu wa Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: