Hakika ilikuwa ni jumapili ya mitihani na huzuni zilizogeuka kuwa faraja

12:05:00 Unknown 0 Comments

Picha hii ni kutoka katika mfululizo wa hadithi ya kademu ka mizinga... angalia  Hapa

Jumapili moja asubuhi Gwantwa akiwa anajiandaa kwenda kanisani akagundua ya kuwa alibakiwa na shilingi 15,000 tu.

Akafikiri na kuona ni vyema atumie 1000 kwa ajili ya nauli na 4000 kwa ajili ya sadaka na ile 10,000 aitunze kwa ajili ya mahitaji yake ya pale chuo kwa wiki ifuatayo.

Akaenda kanisani na wakati anarudi akiwa njiani akapokea simu kutoka kwa mdogo wake wa kike ambaye naye yuko chuo kingine akisema hana hata hela ya kula hivyo anaomba msaada.

Gwantwa alifikiria na kumtumia 6000 ili yeye abaki na 4000 imsaidie kwa wiki ya pili yake na mdogo akamshukuru sana.

Alipofika nyumbani akaona mlangoni kwake kakaa maka mmoja aishie nyumba ya pili akisema nimekaa hapa kwa muda nikikusubiria, tafadhali nisaidie leo sina hata unga wa uji wa wanangu tafadhaki.

Gwantwa akatoa shilingi 3000 na kubakiwa na 1000 bila hata ya kujadili na kuachana na mama yule akifurahi na kuondoka zake akionyesha uso wa furaha na wenye matumaini kwa watoto wake.

Siku ya pili Gwantwa akapokea email kutoka kwa kaka yake aishie uhispania akimwambia kuwa amemtumia kupitia western union kiasi cha shilingi 2,000,000/- zimsaidie katika kuukamilisha mwaka wake wa mwisho pale chuoni.

Gwantwa alifurahi na kumshukuru Mungu kwa hilo na akakumbuka ule mstari muhimu katika kitabu kitakatifu usemao, " UMEBARIKIKWA ULE MKONO UTOAO KWA MAANA UTAPOKEA ZAIDI"

Kwa wale wote wenye mioyo ya kusaidia wenzao bila kujua watapata nini na kwa wale wote ambao wamewahi kupata baraka kwa kutoa basi ni muda wao sasa kuandika neno AMEN na kisha wakashare ujumbe huu

soma zaidi HAPA

You Might Also Like

0 comments: