Post ambayo imegombaniwa na marafiki hapa mtandaoni

10:45:00 Unknown 0 Comments


UJUMBE WA JUMAPILI

Mungu anapokuuliza swali

Nimemwandikia ujumbe huu rafiki yangu sana ambaye anapita katika kipindi kigumu cha mpito ya masha yake. 

Nikaona ni bora nikupe nawe
rafiki wa hapa upate kusoma na kuitumia fursa hii.

Tunavyosoma Biblia, Huwa napenda Mungu anavyouliza maswali. Hajiulizi yeye hapana ila
yeye huwa na majibu ya maswali hayo. Bali hutuuliza sisi kwa kuwa hutaka sisi tupate uelewa wa maswali na majibu yake na
kuyafanyia kazi.

Alimuuliza Adamu, "Uko wapi?"

Kuna kipindi huwa hatujui tuko wapi katika Maisha yetu ya kawaida hivyo twaitaji sauti ya MUngu kutukumbusha wapi tulipo na kuweza kupata nguvu za kuishi vyema..

Alimuliza Musa, "Nini umekibeba mikononi mwako?" 

Mara nyingi kila tunachokihitaji na baraka nyingi tayari huwa mikononi mwetu lakini bado huwa ngumu kwa sisi kutambua hilo.

Alimuuliza Malaki, "Mtu anaweza mwibia Mungu wake?"

 katika Maisha ya sasa imekuwa rahisi sana kwa sisi kutumia muda wetu kwa kila jambo lakini tukamsahau Mungu.

Alimuuliza Ezekiel, "Mifupa hii inaweza ishi?"

Kuna wakati unaweza pita katika nyakati mbaya
nakujiona kama mfu lakini Mungu
anakukumbusha kuwa bado uko salama na mambo bado mazuri kwako.

Alimuuliza mtu aliyepooza, " Unataka kupona??"

Mungu tayari anajua unahitaji kupata ahueni ya Maisha yako ila anasubiri kwanza wewe ulione
hilo na kulitamka kwa kunywa chako.

Alimuuliza Abraham, "Kuna jambo lililo gumu kwa Mungu?"

Nafikiri unavyozidi kuendelea kuishi katika dunia hii. Hata kama mambo yakawa magumu au
yakutisha kiasi gani, hakuna jambo linalomshinda Mungu.

Nakuombea wewe leo na rafiki zako na ngudu zako muwe na usiku mwema

Jumapili Njema

Fuledi

You Might Also Like

0 comments: