Jamaa aua saba kwa mpigo.......... Facebook bwana itamaliza wengi
Kulikuwa na kijana moja aliyeitwa Chaupele,aliitwa hivyo kutokana na kuwa na vipele miguuni,siku moja akiwa amekaa nzi wakaanza kumsumbua na kukalia kwe vidonda vyake miguuni,alichofanya siku moja wakati nzi wananyonya kidonda akawachapa kwa mikono na kuua nzi saba kwa mpigo,basi akaenda kwa fundi nguo ili ashoneshewe kanzu iliyoandikwa "Nimeua saba kwa mpigo".
mara nchi ikavamiwa na mijitu mikubwa miwili wanaoishi msituni,hayo mijitu yaliwaua wanajeshi,basi mfalme akatangaza atampa cheo atakayewaua ila watu waligoma na kumwambia mfalme kuna mtu " aliyeua saba kwa mpigo"umtafute atatuokoa na hili balaa, wao hawakujua Chaupele aliua nzi saba kwa mpigo,basi mfalme akaagiza aletwe mara moja.
Chaupele aliletwa kwa mfalme,na kukabidhiwa mkuki na manati ili aende kupambana na mijitu hiyo miwili msituni,akaanza safari kuelekea msituni,ilikuwa ni usiku wenye giza alipochoka akalala juu ya mti wa matunda,mara usiku wa manane akiwa juu ya mti akasiki mijitu yale yanakoroma huku yamelala,mara yakaanza kuamka taratibu.
Alipoona mijitu yameanza kuamka akalichuma tunda na kuliweka kwenye manati,kisha akamlenga jicho jitu moja kwa maana macho yao yalikuwa yanang'aa kwenye mbalamwezi,jitu akampiga mwenzake ngumi na kumwambia aache uchokozi,wakatulia kwa mda kisha chaupele akamlenga tena mwingine jicho,mara wakaanza kupigana na kuchomana visu,moja akafa mwingine hoi na chaupele akashuka juu ya mti na kummaliza aliyebaki.basi jamaa akapewa cheo cha ulinzi.mara akatokea tena simba mla watu,jamaa akaambiwa aende msituni amwue,na akiweza anapewa binti wa mfalme awe mke wake,chaupele alipofika msituni akaingia ndani ya nyumba mbovu na kuketi,mara simba anaingia mlangoni,je atafanyaje na simba ndo yupo mlangoni?-
Chaupele aliruka dirishani mpaka nje na kuuvuta mlango kwa nje na kumfungia simba ndani,halafu akaenda kwa mfalme na kumwambia kuwa amemkamata simba mzima mzima,alikuwa anakunywa maji halafu akamkamata mkia na kumchapa viboko mgongoni mpaka simba akatii amri,mfalme alishangaa sana.chaupele akaweka sumu kwenye nyama na kwenda kumrushia simba kupitia dirishani,simba alikula nyama akafa.chaupele akaozeshwa binti wa mfalme.
Alipomwoa binti wa mfalme vijana wengi walikuwa na wivu na kupanga jinsi ya kumwua ili wamchukulie mke wake,walikodi majambazi 28,majambazi 28 walizunguka nyumba ya chaupele usiku wa manane.
Kumbe mke wa chaupele alishapata tetesi kwamba wamezungukwa na majambazi,akampa taarifa mmewe,kwa vile chaupele anafahamu wamezungukwa mara akaanza kuongea kwa sauti ili majambazi yasikie,akaanza kuropoka,"MKE WANGU NASIKIA TUMEZUNGUKWA NA MAJAMBAZI 28,NILIUA SABA KWA MPIGO,JE KWENYE 28 NITAUA SABA SABA NGAPI?MKE AKAJIBU "UTAUA SABA SABA NNE"CHAUPELE NAYE AKAJIBU,KWAHIYO NIANZE NA SABA IPI?
majambazi waliposikia huo mjadala wakakimbia mana hawakujua ataanza na saba ipi.chaupele na mkewe wakaishi kwa amani.
share kama umeipenda Tabasamu na Fuledi
0 comments: