Jamani kwa nini mimi????? Akaunti nyingine feki ya facebook imeniharibia ....

06:38:00 Unknown 0 Comments



Uhusiano ulianza kiutani sana kwani mimi tangu nijiunge facebook sikuwahi kuwa na rafiki yoyote yule ambaye ni matawi ya juu au hata yule tu aliye maarufu katika fani tofauti.

Jumatatu moja asubuhi nikiwa na uchovu wa kazi za hapa na pale na ukizingatia bado kichwa kilikuwa na uchovu wa weekend nikaona nipoteze muda kitogo kwa kujisomea upuuzi wa facebook hasa haka kaukurasa ka Fuledi.

Kitu cha kwanza tu baada ya kufungua ilikuwa ni kuzitazama baadhi ya friend request kutoka kwa marafiki kwani ni muda nilikuwa sijawahi pitia anga za facebook. Na mara nyingi hupenda kumkubali mtu ambaye nina connections nae au ana watu ninaowafahamu.

Kuna mtu aliyeomba urafiki akanifanya nipoteze dakika kadhaa za kumtazama vyema ili nijiridhishe kama ni yeye kweli. Maana kuombwa urafiki na mtu maarufu kama Wahu Kagwi ambaye ni msanii maarufu wa mziki huko nchini kenya ni jambo lisilo na masihara.Nikam-accept haraka na kumtext
 hello sisy.... 
I love your music ... 
uko juu sana... 
thansk for addn me.

Zikapita siku na wiki kadhaa bila ya majibu yoyote yale toka kwa mwanadada wahu.

Siku moja nikiwa home majira ya jioni niko busy nachat na marafiki mara ukaingia ujumbe hapa FB na kucheki ni kutoka kwa WAHU, whaaaaaaat nilifurahi sana na kuchati nae.

Mwasiliano yakaendelea kupamba moto na baadae ikanilazimu nianze kuwa mfuatiliaje wa nyimbo zake sana sana yaani ili nisikose la kumwambia tukichati asije ona kuwa mimi sio shabiki wake kipenzi.

Tuliendelea kuchati mpaka ukurasa ukabadilika na taratibu tukaanza kuwa wapenzi na hofu yangu ikawa je Mmewe ambaye ni mwimbaji maarufu aitwaye NAMELESS ambaye pia mimi nazikubali sana nyimbo zake kama angedaka angeweza kunifanyia umafia wa mombasa na pia kwa kuwa mimi ni shabiki wake niliona kama nitamkosea kwa kufanya hivyo lakini mwishowe nikapiga moyo konde tena kwa konde la kiume na kusema kama mbwai mbwai tu nikasonga na mishe.

Binti akazidisha mapenzi mara anipe ratiba za show zake mara hivi mara vile na hatimaye kuna siku nikasikia kuna kampuni moja inamleta hapa bongo kupiga show nami nikawahi tiketi mapemaaa na yeye akaniambia atakuwepo na nitapata nafasi ya kuongea nae tena sana.

Siku ya show nikaenda na nikajitahidi kukaa sehemu nimwone na pengine apate nafasi ya kuniona lakini akanitext kuwa protocal zimemzingua na kuwa hawezi tena ila kwa kuwa akimaliza show siku ya pili atanitext wapi niende tuonane nikaona imekaa vyema na kuamua kuondoka zangu.

Siku ya pili nikawahi kuamka na kujiandaa na kwenda kwa rafiki yangu Nolesy kuomba gari akasema hana ikanibindi nimpigie Mtafya anipe namba ya Nasri ili aniazime gari bila mafanikio mpaka pale Trio aliponipa msaaada wa namba ya Nasri ambaye akanipa gari kwa masharti nisiligongeshe.

Mida ya saa saba na nusu nikawa nimefika maeneo ya Dagaa Dagaa pale Shekilango, ingawa hofu ikawa amejuaje maeneo yale? Nikajisemesha huwezi jua pengine promota aliyemleta alimpangishia hotel labda pale maeneo Rombo hotel.

Nikafika dagaa dagaa na kumtext kuwa nimefika nipo meza ya pembeni mlango wa kuendea uani hapa, robo saa akaingia kijana mmoja wa kiume ambaye ni baunsa ila ana mikogo zaidi ya mabinti wa sasa akakaa pale na kunisalimia kwa jina langu, nikamjibu huku nikiwa namshangaa kanijuaje jina? Akaniambia handsome tafadhali usichukie wala kusema chochote.

Mie mwenyewe ati ankoli napendelea sana Nyimbo za huyu Mwanadadaa, na huwa zanipa rahaa utamu nikimsikiliza sasa usichukie kwa vile umeniona ni wa jinsia tofauti yake mimi nimeweka ile profile id kwa kuwa i love much her works..... I love you pia hun huku akitaka kunishika shavu

(Muda huo watu wote wananishangaa mimi na jasho la hasira lanitoka)

Nikainua glasi yangu na kumalizia  Viloba nilivyomiminia humo kabla ya kuinuka na kumpa konde moja la uso kabla ya walinzi kunivuta na kunitoa nje huku watu wakicheka pale na wengine wakionyesha kuchukizwa na huku yule kijana akipiga kelele dia rudi dia rudi na hatimaye kuondoka huku nikiona mwaka 2014 nuksi gani zaniandama mimi kijana wa watu?

Mpaka sasa sijui yule kijana aliamua kufanya vile kwa nia agani.... kweli facebook ni sawa na usiku wa giza... huwezi jua nani ni nani mpaka yakukute

Kwa sasa naamini page tu za wasaninii tu na sio akaunti binafsi...

Shiti i heti fesibuku

Soma mwendelezo wa kisa hiki kwa kubofya HAPA

You Might Also Like

0 comments: