Kama njia hii ni bora iga mapema kabla hujakumbwa na dengue wa huzuni

14:17:00 Unknown 0 Comments



Majirani wawili Mtafya na Nolesy walijenga nyumba mtaa mmoja na zikawa zinatazamana na
kugawanywa kwa uzio wa miti.

Nolesy yeye ni mfugaji alikuwa na mashamba ya mifugo na pale nyumbani alifuga mbwa wawili
ambao kila usiku walipiga sana kelele kila walipohisi kuna watu wakizinyemelea hizo nyumba mbili.

Mbwa wale walifanya kazi yao ya ulinzi na kweli nyumba zile zukaogopwa sana ingawa Mtafya
alichukizwa sana na zile kelele za mbwa wa nyumba ya jirani.

Kwa hasira na kinyongo akaamua kwenda kutoa malalamiko yake kwa Nolesy na baadae kwenda
kwenda katika vyombo vya sheria.

Kesi ikaunguruma na na baadae mahakama ikatoa uamuzi wa mbwa wale wote wauawe kwa
kosa la kusababisha kelele kwa majirani.

Nolesy alilia sana akiomba wasifanye hivyo na mwishowe mbwa wale wakauawa na mtafya
kuondoka kwa furaha kwani lengo lake limetimia.

Miezi na miaka ikapita baadae Mtafya akapata baraka ya mtoto katika nyumba yake na mtoto
yule alikuwa akilia sana usiku kiasi cha kuwafanya majirani wakose raha kabisa na kelele zile.

Nolesy akaenda kwa mtafya kumwomba kelele zile ziishe lakini mtoto akazidi na hatimaye nolesy
akaenda mpaka mahakama ile ile na kuwasilisha malalamiko.

Mtafya akaitwa na kesi ikaunguruma kwa siku kadhaa na hatimaye ikatolewa hukumu ya mtoto yule kuuawa pia.

Mtafya alilia zaidi ya siku kadhaa kaiomba adhabu ile iepushwe na mahakama ikasema mwenye
uwezo wa kutengua uamuzi huo ni Nolesy kama ataamua.

Nolesy alikuwa mgumu na mtafya kwa siku zile yeye na familia wakaanza kudhohofika kwa
mawazo mpaka pale Nolesy alipotamka kuwa ameamua kulifuta shauri lake pale mahakamani na mtoto ana haki ya kuishi kama viumbe wengine hivyo asiuawe.

Ndugu zangu, tusiwe wepesi wa kuhukumu huku nasi tukiogopa kupewa hukumu kama hiyo kwa
kiwango kama kile kile tulichopimia wenzetu.

Usihukumu au kumfanyia mtu kitu ambacho zamu yako ikifika nawe utaumia na kulalamika kama unaonewa na kutaka dunia ikupe msaada.

*Kabla  hujamdhulumu mtu jiulize itakuaje kama yeye akikufanyia wewe?.

*Kabla ya kumchafua mtu hebu fikiri wewe ukichafuliwa utajisikiaje?

*Kabla ya kumsaliti mwenza wako jiulize je maumivu hayo nawe ungepata ungeyakabili vipi?

*Kabla ya kumlaumu rafiki kwa kinyongo jiulize je angekufanyia wewe unge feel vipi?

*Kabla ya kusema humpendi mama, baba, rafiki, mchumba hebu jipe muda wa kufikiri je wewe
ukiambiwa hivyo au kufanyiwa hivyo utalipokeaje?

Maisha ni sawa na mpira wa miguu kamwe usitegemee kuwa utabaki kileleni miaka yote, kuna nyakati za kung'aa na nyakati za kufubaa.

Mungu wetu hutuoa baraka za kila aina na huwajibu maadui zetu kwa namna za ajabu kama mtafya alivyopewa funzo la maisha na sasa ni mchungaji

Mungu atujalie mioyo yenye busara na hekima jinsi kuishi na mbwa mwitu waliojivalia ngozi ya
kondoo.

like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: