Wooooow!!!! Fuledi ashida tuzo na kukabidhiwa zawadi ya gari..... ASANTENI MARAFIKI WANGU KWA KURA ZENU

14:01:00 Unknown 0 Comments



Jumatatu ile Fuledi aliamka akiwa na uchovu wa pombe za jumapili ya na yake, ilimlazimu kutumia njia ya kunywa pombe ili angalau aweze sahau kurupushani za kulipa ada pamoja na baba mwenye nyumba ambale alishakuwa katema mikwara kibao ya kuchukua nyumba yake kama malipo ya pango yasingefanyika mapena kabla ya wiki ile kwisha.

Fuledi akakumbuka kuwa siku hiyo gari la ofisi lisingekuja kumchukua kwani dereva wao anaumwa na yeye akaona awahi ili atembee kupitia vichochoro viwili vitatu ili awahi majukumu ya ofisini kwa silku hiyo.Hivyo akajiandaa haraka na kuanza safari yake.

Akapita katika uchochoro mmoja na kwa mbali alisikia sauti ya mtu aliyekuwa akiita kwa taabu katika kijibonde fulani ikambidi achungulie na baada ya kufika pale alimkuta mama mmoja ambaye alikuwa kaumizwa vibaya sana na damu nyingi zimeganda na nyingine zikiendelea kuvuja ilionekana kama alivamiwa na kutupwa hapo usiku.

Fuledi akawaza afanyaje, duuh kwa akili ya haraka akapiga simu polisi na polisi wakaja na wakamchukua yule mama na kumpeleka Hospital mapema na kuanza matibabu, mama yule kwa hakuwa anaweza kuongea tena basi ikambidi fuledi aanze kuumiza kichwa juu ya nani wa kumfahamisha. Kwa bahati nzuri yule mama alikuwa na kajitabu kadogo fuledi alikachukua na kuona kuna baadhi ya namba ikambidi aaze machakato wa kumtafuta mtu wa karibu na kwa bahati nzuri mmoja alikuwa mtoto wa mama yule.

Baada ya dakika chache familia ya mama yule ilifika na kweli walionekana watu wenye fedha zao basi fuledi akawasimulia alivyoona na wakamshukuru na hatimaye wakamsaidia fuledi aende kaazini mara moja kwa kumpeleka huku mgonjwa akiendelea na matibabu.

Fuledi alifika kazini na kusimulia mkasa ule na wenzake wakamsifia na kumpa hongera kwa ushujaa ule kwani wengi wetu tungekimbia kuogopa kesi. Basi kila siku asubuhi na jioni fuledi alimtembelea mgonjwa mpaka alipo ruhusiwa kwenda nyumbani, wote wakamshukuru sana fuledi kwa ukarimu na uzalendo wake.

Wiki moja baadae baada ya mama kupona kabisa familia ile iliandaa sadaka ya shukrani kwa ajili ya kumshukuru MUNGU wao kwa kumwokoa mama yao ambaye alivamiwa na genge la majambazi wakati akijiandaa kufunga duka lake ya vitu vya thamani na kumwibia kila kitu gari lake, fedha, na nyaraka kibao kisha kumtupa katika bonde la ajabu.

Baada ya kutoka kanisani walirudi nyumbani ambako watu wengi walikuwa wamealikwa ndugu jamaa na marafiki wa familia ile. Mambo yalipamba moto katika kajiukumbi kale kabla ya DJ kuzima mziki na MC kutangaza kuwa fuledi alihitajika kusimama na kwenda mbele.

Fuledi alipofika pale baba wa nyumba ile aliongea maneno machache ya kumshukuru na kusema kuwa familia ilikuwa imeandaa suprize kwa ajili yake. kama zawadi kwa msaada wake kwao.Baada ya kuongea maneno hayo walimpa cheki ambayo ndani yake ilikuwa na milioni ishirini, funguo za gari dogo aina ya VEROSA na hati ya nyumba ya kuishi..... Fuledi alianguka chini kwa mshangao na kisha kuzirai pale pale na kukimbizwa hospital.

Fuledi alipozinduka akaona kazungukwa na manesi na baadhi ya rafiki zake wakiwa na nyuso za majonzi, kwa taratibu akauliza "jamani kwa nini niko hapa?" dada yake wa karibu aitwaye Antonia milinga akamwambia "jana ulikuwa kwenye promosheni ya konyagi ukanywa konyagi nyingi wakati wa shindano la nani mkali wa viroba ili apate laki tano, na wewe kufika kiroba cha saba ulianguka chini na kuzimia wote tukajua umekufa ndio tukakuleta hapa"

Fuledi hakuamini kuwa ile cheki ya na milioni ishirini, funguo za gari dogo aina ya VEROSA na hati ya nyumba ya kuishi ilikuwa ni ndoto wakati akiendelea na matibabu.

Fuledi mpaka leo bado hana ajira na anaendelea kusaka ajira

You Might Also Like

0 comments: