Ujumbe kutoka kwa admin wa Tabasamu na Fuledi
Hello Rafiki,
Ni furaha kubwa kuona mtandao wetu unazidi kukua na kupendwa na marafiki wapya kila siku.
Nitumie fursa hii pia kukuomba uzidi kushirikiana nami katika kuhakikisha tunafurahi, kuelimishana na kufahamiana zaidi kama lengo kuu la mtandao huu bila ya kuathiri utamaduni wetu..
Pia naomba kwa post ambayo mtu utakereka au kukwazika tuwasiliane kupitia whatsapp 0713317171 au tabasamunafuledi@gmail.com ambapo pia waweza toa wazo la post mpya.
Kwa upande wa wasanii walioibuka washindi katika tuzo za Kili Music Awards, naomba niwape pongezi na kuwapa salamu za hamasa na shauku ya kuongeza juhudi zaidi katika kuitambulisha sanaa ya taifa letu kimataifa zaidi.
Na sisi mashabiki tuzidi kuwapa nguvu michango yetu ili nao wajivunie kuwa na sisi.
Nawatakia siku njema marafiki zangu wote.
Fuledi
0 comments: