Ukiwa mtandaoni epuka mambo haya na kuyakimbia kabisa

12:18:00 Unknown 0 Comments



1. Usiwe mwepesi wa kubofya kila link unayotumiwa inbox, nyingi huchukua taarifa zako za siri

2. Usiifuate link itakayokuuliza password yako au kukuomba kuchukua taarifa zako ukakubali kama huifahamu vizuri

3. Usiingize taarifa zako za siri kama vile bank account, password zake na za mitandao ya simu pia

4. Mtu akikuomba uifuate link yake na kumpigia kura hata kama anakufahamu nawe wamfahamu hebu mpigie simu kwanza kumuuliza wengi wanakuwa wameshaibiwa akaunti zao na mtu mwingine anatumia kutaka kuiba yako pia

5. Asikudanganye mtu kuwa kuna website ukijiunga itakupa dola nyingi kwa siku, huo ni wizi hebu fikiri ni tajiri gani anaweza kukushirikisha amegundua shimo la dhahabu nyumbani kwake?

6. Mtu anakutumia ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu wakati hujawahi kushiriki hebu fikiri kwa makini hao jamaa wanampango gani na wewe?

7. Binti yuko kambi ya wakimbizi na anadai ana fedha anataka akutumie wewe umtolee, hebu jiulize kwani wewe uko kambi moja na huyo mkimbizi au wewe ni mkimbizi mpaka akufahamu?

8. Mtu hujawahi onana nae na sio rafiki ila anadai kuwa anaipenda profile picture yako nawe kwenye profile kuna picha ya mtoto wako, inamaa anakupenda wewe au mtoto wako?

9. Hakikisha password yako iwe ni machangabyiko wa namba na ferufi na alama kama ! na nyinginezo

10. Epuka kabisa roho itakayokupa kiburi cha kutoisoma Tabasamu na Fuledii na kukomenti

Kwa ufupi hakuna hela za bure online, watu wanalia usiku na mchana wapate watembeleaji wengi kwenye web zao ili wapate matangazo na wanashindwa … wewe unadanganywa kirahisi kuna hela za bure hapa…. Si watu wasingelia njaa mitaani?

Acha umbulula hebu fanya kazi haraka na kujipatia kipato

You Might Also Like

0 comments: