wife atumia akaunti feki ya fb na kumfanya mme wake kumtajialist ya mabinti wote aliotmbea nao
Leo asubuhi nimeingia kazini mapema sana kuliko kawaida yangu baada ya kugombana na wife home.
Nilipofika nikatulia kwenye computer na kuwa busy na mitandao ya kijamii kujipa nafasi ya kusahau maugomvi.
Ile kufungua facebook tu nikakutana na friend request ya binti mmoja mtamu sana mwenye pic za kuvutia na kuanza kuchati naye.
Kwa kweli binti yule anajua sana kuchati na huwezi amini mpaka kufikia mida ya saa nne nilikuwa sijafanya kazi yoyote pale ofisini kwa utamu wa text zake.
Tukazidi kufahamishana na yeye akadai ana mme anaye pendana naye sana na mimi nikawa namwambia nina mke ila ana longo longo sana hivyo simpendi kiviiile ni basi tu yaani.
Tukaendelea kuchati na akawa anaonekana anasogea sogea kwangu na akaniuliza niwe muwazi kumwambia kama tangu nuanze ndoa kuna wanawake nimewahi tembea nao ndio anikubali kuwa nae kwani anaogopa magonjwa, nikampa idadi yake bila kusita na hata alivyoomba majina yao nikampa yale ya mwanzo tu.
Akanipenda sana kwa kuwa muwazi na kuniambia atafikiria kwa kuwa mimi ni mkweli sana.
Baadae nikamwomba afanye tuonane akanipa namba ya voda nami baada ya kufurahi nikamwambia ningempigia jioni hii.
Jioni hii nimeipiga ile namba sauti ni ya mke wangu na nilipojaribu kumtumia fedha kwa mpesa, nimeishiwa nguvu kuona ni jina la mke wangu na hakuwa na laini ya voda kabla.
Jamani nimetoka kazini nipo hapa bar nakunywa na sijui leo nyumbani itakuwaje...:..
Naombeni ushauri vijana wenzangu kwani hapa kati nimekuwa mkorofi sana kwa mke wangu na akasema kuna siku atanibamba tuu.....
Naumia zaidi ile kutoa list ya mabinti niliotembea nao wote....
Nahitaji ushauriwa akili imesizi....
soma comment za wadau hapa
0 comments: