Akasimulia kisa changu na kila mtu alilia na baada ya hapo akanipa hati ya ile nyumba niliyokuwa niliisimamia na mbele yake ililuwa na vyumba 15 vya kupangisha.

20:58:00 Unknown 0 Comments

Niliamka na kukaa kitandani nikiwa nimeinamisha kichwa kwa zaidi ya dakika 20 huku nikiwaza mambo mengi sana.

Nikamkumbuka marehemu baba yangu ambaye akikufa mwezi mmoja kabla ya mtihani wangu wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne.

Kama haitoshi nikakumbuka jinsi nilivyokuwa najitahidi darasani na baadae kuja kupata ziro kisa mawazo ya kifo cha baba ambaye alikuwa msaada wetu.

Nikakumbuka zaidi jinsi mama alivyokufa miezi minne baada ya baba kufariki kwa shinikizo la damu baada ya kutaka kutolewa katika nyumba ya shirika tulimokuwa tukiishi.

Nikaangalia picha ya mdogo wangu wa pekee ambaye kutokana na ugumu wa maisha na bila msaada aliamua kuolewa akiwa na umri wa miaka 16 na kuacha ndoto ya shule.

Huku machozi yakinitoka mara hii nikaanza kuumia jinsi ambavyo nafanyishwa kazi ngumu katika duka la mangi na kisha mwisho wa mwezi kupewa ujira mdogo.

Ndio pamoja na kuniamini na kila siku mchana kunituma benki kwenda kumwekea fedha za mauzo zaidi ya milioni nne kila siku lakini bado vile vicheko vya marafiki zangu kuniita msukule bado vilijirudia kila mara.

Tangu nianze kazi hiyo miaka 15 iliyopita ni mimi peke yangu mkongwe niliyobakia wengine waliiba na kukimbia bila kushikwa na baadhi wako gerezani baada ya kushikwa na mangi.
Nikajikongoja kwenda bafuni ili nijiandae kwani siku hiyo nilitakiwa kuwahi kwenda kusimamia ujenzi wa nyumba yake mpya na kuwalipa vibarua.

Nikiwa njiani naelekea ofisini nilajisemesha kuwa leo lazima nikimbie na fedha angalau nikamtafute mdogo wangu na kuishi nae ambaye kwa sasa alikuwa kaachika na anafanya kazi katika danguro moja maarufu kama mama ntilie jambo ambalo hata baba na mama wangekuwa hai wasingeweza kuliruhusu kamwe.

Nilifika ofisini na kukabidhiwa fedha zaidi ya milioni sita za vifaa na malipo ya vibarua wale.
Nikapanda daladala na baada ya kufika mwisho nikapanda bajaj na nikiwa nawaza kukimbia huku roho yasita mara kwa mbali nikaona mama mmoja aliyefanana na marehemu mama yangu nikazama kumwangalia na kupitiwa na mawazo kabla ya kushtuka tumefika na mpango ukawa umekufa.
Nikafika pale nikalipa na kuchukua gari la kwenda kufanya manunuzi na kumaliza kazi kisha kurudi ofisini ambako nikaona wafanyakazi wako katika mshangao kuwa mwenzetu saidi alichukua nafasi yangu ya kwenda bank kupeleka hela na akataka kukimbia nazo akashikwa na walinzi wa siri wa boss na sasa yupo ndani.

Kuanzia hapo sikuwa tena na wazo la kuiba na kuanza kutunza fedha zangu ili nianze biashara ya duka dogo na ya kumtafuta dada

Baada ya kukaa miezi kadhaa nikawa nimefanikiwa kuweka milioni moja na nusu nani nikaona yanifaa kabisa.

Nikaenda kwa boss na kumwomba kuwa mwezi ujao nitakuwa natimiza miaka 20 ya kufanya kazi nawe. Naomba uwe mwezi wa mwisho kufanya kwako ili nami nianze kujitegemea.

Boss alifurahia sana mimi kumwambia vile na akaniita mfano bora kwa wafanyakazi wake na kuniomba niongeze miezi mitatu kwani ataenda dubai kutibiwa na baada ya hapo akirudi nitaondoka kwani hana mtu wa kumwamini.

Nikamsubiri na kumeombea apone na baada ya miezi minne alirudi familia yake ilimpokea kwa furaha tukishirikiana na baada ya wiki moja ya kujiona kama yuko sawa kukaandaliwa tafrija nzuri na kumshukuru Mungu kwa kumponya.

Wafanyakazi wote tulihidhuria na baada ya tafrija kunoga baba alisimama na kuwashukuru watu kwa upendo wao na akasema pia leo ni siku ya huzuni na furaha pia kwani kijana niliyempenda akaniita na kusema anaondoka katika kampuni yangu na kwenda kujitegemea .

Akaongeza kupitia maisha ya huyu kijana amenifundisha kupenda kidogo na kukifurahia, kuwa na furaha hata pale dunia inapokuwa mzigo kwako na kuona umebarikiwa hata kama hujui hizo baraka.

Akasimulia kisa changu na kila mtu alilia na baada ya hapo akanipa hati ya ile nyumba niliyokuwa niliisimamia na mbele yake ililuwa na vyumba 15 vya kupangisha.

Sikumbuki nilishukuru vipi ila siku ya pili yake nilianza kuzitumia zile fedha zangu kumtafuta dada yangu.

Nilibahatika kuonana naye akiwa katika hali ngumu na mtoto wake na sasa tunakaa wote tumepangisha vile vyumba na tukeanza kusoma masomo ya jioni ili ndoto ya shule iendelee.

Mungu zilaze pema peponi roho za marehemu baba na mama.

Soma kisa kingine HAPA

You Might Also Like

0 comments: