Facebook yamtokea puani binti mwingine................................
Trice alianza kuitumia akaunti ya facebook kwa shinikizo kubwa kutoka kwa marafiki zake ambao wakati huo wao walishakuwa maarufu fb.
Ilimchukua mwezi mmoja tu kujikuta akishindwa kuongeza marafiki kwani alifikia idadi ya mwisho ya kiwango cha marafiki na waliotaka kuwa rafiki nae hawakuwa na la ziada zaidi ya kuwa followers.
Kutokana na ubora wa picha zake alifanikiwa kuwavutia vijana wengi na miongoni mwa vijana hao alikuwa ni kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Majuto.
Majuto na Trice walianza kuchati kama marafiki wa kawaida kabla ya urafiki wao kufungua ukuasa mpya na majuto kuwa kama baba mlezi wa trice.
Kila alichohitaji trice alitumiwa na kama haitoshi kiwango cha fedha alichokuwa akitumiwa na majuto kwa ajili ya kujikimu kilikuwa zaidi ya mara mbili ya mshahara wa mfanyakazi wa kawaida.
Maisha yakawa vizuri na kila mtu akamfurahia trice kwa kupata bahati hiyo wengi wakamfananisha na mchimba mbadini aliyefanikiwa kujigundulia madini nyumbani kwake kuwa ataweza kuchimba na kuuza muda wowote ule atakao.
Ila kuna jambo moja ambalo lilimfanya akose raha kwani pamoja na kupigiwa simu na hata kutumiana picha kwa njia ya whatsapp na facebook ila hawakuwahi kuonana.
Trice akaomba wapange kukutana lakini majuto akaomba ampe muda kwani bado kuna kazi anazifanya na pia alitamani wakikutana ampe surprise fulani hivi. Trice alikubaliana na hilo.
Siku zikaenda hatimaye trice akasafiri na rafiki yake kwenda mpaka mji aliopo majuto na walipofika pale wakapokelewa na dereva wa majuto na kupelekwa nyumbani ambako aliwapokea na hatimaye wakakaa pale na kupata chakula cha pamoja kabla ya mary kuomba aende akalale hotel iliyopo jirani.
Usiku mary akawa kila akitaka kulala moyo wake unagoma na kwa wakati huo kule kwa majuto, trice akawa kaingia chumbani na majuto na mwili ukawa ukimsisimka kama vile sio chumba cha kawaida.
Majuto akamwambia fungua kabati kuna surprise yako, kwa furaha trice akiwa na furaha akafungua kwa butwaa kuna toy kama la kuchezea watoto likamrudia na kuanza kunyonya ziwa lake la kushoto akapiga kelele ingawa hakusikika na majuto akatoka na kuwasha gari aondoke.
Wakati huo mary akawa kasogea karubu na nyumba ya majuto na zile kelele alizisikia japo hakujua ni chumba gani ila akaingia na kuona trice kaishiwa nguvu na yule toy akitaka kurukia ziwa la pili.
Mary akasali kimoyo moyo na kumtoa yule toy ingawa alikuwa na nguvu na hatimaye akafanikiwa kutoka na kwenda hotel nyingine.
Siku ya pili walirudi kwao baada ya kupeleleza na kuambiwa ya kuwa majuto hutumia utajiri wa ndumba na kama yule toy (mdori) angenyonya na ziwa la pili basi angekufa pale pale.
Ilimchukua zaidi ya miezi kumi mpaka akili kumrudia vizuri trice baada ya kupata maombi na yeye kumrudia Mungu wake na sasa amefungua chuo cha mambo ya mitandao ya kijamii akitoa elimu ya namna ya kufaidika na mitandao hiyo na mambo ya kuyakwepa.
Rafiki wa fuledi nakuombea kuwa kila rafiki utakayekutana naye hapa facebook au katika mitandao mingine ya kijamii awe mwenye nia njema nawe kamwe usidakwe katika kila hila ya mwovu shetani na vibaraka wake.
Kila ufanyacho kiwe na hekima nasi tufurahie wewe kuwa rafiki yetu pia.
0 comments: