Kudadadeeeek!!!!: BUNDI ameingia kwenye kambi ya timu ya Ghana nchini Brazil

15:33:00 Unknown 0 Comments


. Wakati taarifa za fedha kupelekwa kambini kwa mbwembwe za aina yake zingali za moto, wachezaji wawili wametimuliwa kambini humo.
Taarifa kutoka nchini Brazil inakoendelea michuano ya Kombe la Dunia la FIFA zinadokeza kuwa Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng waliamriwa wawe wameondoka kambini hapo ifikapo saa mbili asubuhi ya leo, kwa saa za Brazil.

Wakati Ghana ikitarajiwa kumenyana na Ureno baadaye leo katika mchezo wa mwisho wa kundi G, wachezaji hao wametimuliwa kutokana na kupigana kwao kulikotokea juzi. Vyombo vya habari vya kimataifa vimeendelea kuripoti kuwa, baada ya ugomvi huo Muntari aliwatukana pia maafisa wa timu hiyo ya taifa.

Muda mfupi uliopita, kocha wa Ghana Kwesi Appiah amethibitisha kufukuzwa kwa wachezaji hao.
Habari hii ni kwa mujibu wa magazeti ya nchini Ghana.kama ilivyotafsiriwa na Fadhy Mtanga

You Might Also Like

0 comments: