NI WANGAPI WATAPITA BILA KUSOMA KISA HIKI CHA KWELI?

20:29:00 Unknown 0 Comments



Mama mmoja aliewalea watoto wake kwa taabu sana na wakawa wamefanikiwa kimaisha ingawa wote walikuwa hawamkumbuki, siku moja alipatwa na na tatizo akiwa shambani na kuvunjika miguu yote miwili.

Kwa haraka ikabidi awaombe waliokuwa wakimuuguzia nyumbani watoe taarifa kwa vijana wake wapendwa ili waje japo kumpa fedha ili atibiwe na kuweza kuwa mzima tena.

Baada ya kulazimishwa sana wale watoto waende kumwangalia mama yao, mmoja wao akaamua aende ili kumaliza kelele za ndugu na wengine kuendelea kuta bata huko walipo.

Akawasha gari yake aina ya Jeep na kwenda mpaka huko mkoani Mbeya. Kufika pale mama alifurahi sana na kumwambia mwanawe kuwa alihitaji msaada wake kwani bado alihitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi ingawa alishindwa fedha.

Yule kijana kwa dharau na jeuri aliyokuwa nayo alisema, “ mama wewe ushazeeka sasa na tatizo hili limekufanya uwe kiwete hivyo sioni haja ya wewe kumaliza fedha kwa matibabu, bali wewe baki hapa hapa umalizie siku zako za kuishi”

Yule kijana alimaliza na kuwasha gari akiondoka zake huku akimwacha mama yake machozi yakimtoka na baadhi ya ndugu wamemshikilia wakimsihi amsamehe tu Yule mtoto kwani hajui alitendalo.

Jioni ya siku ile Yule kijana akiwa ametoka bar kunywa ili akijiandae kwa safari yake ya kurudi dar, alipatwa na ajali mbaya sana ambayo mpaka sasa imemfanya ashindwe kutembea wala kufanya chochote kwani alivunjika mgongo.

Na kwa kuwa yeye pekee ndiye aliyekuwa akiwasaidia wenzake katika biashara zao basi wadogo wakashindwa kusimamia biashara na mpaka hivi sasa wote wako kijijini wakimtegemea mama yao ambaye wasamaria wema walimsaidia mpaka anapona miguu yake.

JAMANI, Kabla hujafa hujaumbika na kumbuka upendo wa mama hauna kikomo, kwani mama Yule aliyeambiwa kuwa ni kiwete na angekufa MAPEMA, leo hii yeye ndiye anamhudumia Yule kijana ambaye ni wakumalizia haja zote sehemu alipo.

Na kama haitoshi wale wanawake wazuri aliokuwa nao pamoja na marafiki wote wamemkimbiana sasa kimbilio lake ni kwa mama yake tu.

Mkumbuke mama yako jioni hii kwa kusema “NAKUPENDA MAMA” kama kweli unamjali

Ruksa kushare

You Might Also Like

0 comments: