Ona jinsi baunsa alivyoumia mgongo kisa mchepuko

13:18:00 Unknown 0 Comments

Baunsa wa night club alienda kutibiwa mgongo kwa doctor.
Doctor baada ya vipimo akamuuliza
baunsa ilikuwaje mpaka akapata mshtuko wa uti wa mgongo.
BAUNSA;Nilipoingia ndani asubuhi nikitokea kazini,nilisikia makelele
chumbani kwangu nikajua mke wangu yupo na mwanaume mwingine,nikazama chumbani
lakini sikumkuta mtu,mara nikasikia mlango wa sebuleni umefunguliwa kwa fujo nilipochungulia kupitia dirishani nikamwona mtu anakimbia
huku anavaa shati nikachukua fridge nikamrushia nikiwa ghorofa ya tatu,hapo ndipo niliposhtua uti wangu wa mgongo.
(Alipomaliza tu kauli yake,akaingia mgonjwa mwingine kaharibika kama kagongwa na gari).
Doctor akamhoji;vp ndugu,nini
kimekusibu?.
MGONJWA;Nilisahau kuweka alarm
asubuhi nikachelewa kuamka kwenda kazini,kazi yenyewe niliajiriwa jana tu baada ya
kukaa jobless kwa muda mrefu,nikatoka nje huku navaa nguo,mara nikapondwa na fridge
kichwani.
{Mara akaingia mgonjwa wa tatu
akiwa na hali mbaya kuliko
waliomtangulia}.
Akaanza kujieleza,'Doctor,mimi
nilikuwa nimejibanza ndani ya fridge,mara ghafla lile fridge likabebwa na kutupwa kutoka
ghorofa ya tatu mpaka chini'.

You Might Also Like

0 comments: