Tiba ya kuacha kukojoa kitandani yazua balaaa. Kweli mbeya kila siku majanga....mgonjwa aikimbia familia

02:15:00 Unknown 0 Comments


Jamaa alikuwa na tabia ya kukojoa kitandani , na akawa akichukizwa na tabia hiyo ambayo pia ilimkosesha raha mkewe hasa waendapo ugenini kwani ilimbidi amwekee alamu mumewe pamoja na kuwa juhudi hizo hazikuzaaa matunda.

Jamaa akaamua aende kwa mganga wa mila ili ampe suluhu la janga hilo.
Jamaa: Bwana mganga mie na tatizo la kukojoa kitandani na ni la muda mrefu sasa.
Mganga: Huwa inakuaje mpaka unakojoa?

Jamaa: Huwa nakuwa ndotoni kisha kuna jamaa huwa ana niikimbiza weeee baadae hufanikiwa kujificha na baada ya jamaa kupita mie kwa hofu huamua kukojoa kisha nirudi nyumbani ndio hapo sasa nikiamka huona nime mwaga radhi

Mganga: Pole sana sasa mimi nitakupa dawa na leo akija tu wewe ndio utamkimbiza na ikimshika mcharaze bakora

Jamaa karudi home na usiku kama kawaida yule mtu akaja na alipoanza kumkimbiza tu jamaa kawa mbabe na kuanza kumtoa nduki mpaka kwa bahati mbaya akaingia kwenye shimo.Jamaa kwa hasira kasema umeninyanyasa sana kwa miaka kadhaa mpaka hadhi yangu imeshuka sasa leo nakunyea huko huko ili ukome kabisa.

Asubuhi jamaa anaamka anaona mkewe analia anauliza nini wangu mke akamjibu angalia aibu uliyonupa mme wangu yaani kutoka kukojoa mpaka unakunya kitandani?
share na like Tabasamu na Fuledi

You Might Also Like

0 comments: