Binti anusurika kufa kisa asali

22:14:00 Unknown 0 Comments

Ilikuwa sio kawaida ya mme wangu kutoka nyumbani siku za jumamosi ila siku hiyo aliniambia kuwa alitakiwa kuonana na rafiki yake hivyo aliwahi kuondoka.

Mpaka mida ya chakula cha mchana alikuwa bado hajarudi nikafikiri labda kakutana na marafiki zake na watakuwa na maongezi yao hasa ukizingatia kuwa ni weekend.

Nakumbuka alirudi mida ya saa moja kasoro jioni na kwa jinsi nilivyomwona alionyesha kuwa kuna kitu kinamtatiza hivyo baada ya salamu nikamwaacha akaingia chumbani.

Robo saa baadae niliingia chumbani na kumshuhudia akiwa analia sana, bila hata ya kuuliza nikajikuta machozi yakinitoka pia na ukizingatia ndio mara yangu ya kwanza kumshuhudia akiwa katika hali hiyo.

Hakuongea kitu zaidi ya kuomba apate muda wa kupumzika kisha kesho yake ataongea. Nilimwacha akiwa amepumzika nami nikaendelea na kazi jikoni ingawa akili ilikuwa haipo sawa kabisa.

Asubuhi aliamka akiwa hana furaha nami nikiwa na hamu ya kufahamu nini kimemsibu lakini nguvu ya kumuuliza iliniisha kwani niliogopa sana kumsababisha atokwe na machozi au akose raha kama jana.

Alinisalimia na kisha akaenda bafuni baada ya muda chai ikawa tayari tukanywa na akaniambia alitamani sana tule chakula cha pamoja na watoto wetu mapacha waliokuwa wakisoma shule ya msingi ya bweni pale jirani na kwetu.

Tukakubaliana na baada ya hapo akaondoka na akarudi akiwa kabeba baadhi ya vitu vya kupika pamoja na watoto akiwa na furaha tofauti na jana yake.

Akaingia jikoni akapika tukisaidiana naye kwa mara ya kwanza baada ya kitambo tangu tupike wote na wote tukawa sasa tuko mezani tunakula.

Tulikula kwa furaha lakini dakika chache baadae mme wangu aliniangalia tena mimi na wanangu na kufuta machozi kisha akasema kuna kitu alitamani aongee na tumsikililize.

Alianza kwa kusema "Jana alienda kwa daktari na amegundulika kuwa figo zake zimeathika na kama hata fanyiwa upasuaji wa haraka na kubadilishiwa figo tena katika hospitali kubwa na kwa ushauri zaidi nje ya nchi basi ataweza kufa muda wowote"

Nilielewa kilichomtoa machozi ni kwamba wakati huo hali yetu kifedha ilikuwa mbaya na kama haitoshi kuweza kuipata fedha kubwa kiasi kile kwa wakati ule ilikuwa sio kazi rahisi.

"Baba utapona tuu usilie" ndio neno kutoka kwa wanangu lililonishtua katika dimbwi la mawazo na kisha nikainuka na kumshika mkono mme wangu na kwa pamoja na wanangu tukasali na nikamhakikishia mme wangu kuwa tutapambana na atapona.

Tulianza kuahangaika kuwapigia ndugu, jamaa na marafiki lakini hakukua na dalili za mafanikio..

Nakumbuka ilifika kipindi nikaanza kuuza vitu vya ndani pale nyumbani lakini bado fedha ikawa kidogo.

Tulirudi kila jioni na kupiga mahesabu tumefikia wapi lakini bado tuliishia kufuta machozi na kupeana maneno yenye nguvu kuwa tutafanikiwa.

Ilifikia kipindi mme wangu akazidiwa na nikampeleka hospitali ambako alikuwa akiendelea na dozi ya kutuliza maumivu wakisubiri fedha ili asafirishwe.

Hakuna shirika la kijamii, kanisa, taasisi mbalimbali hata wafanyabiashara wenye fedha zao ambao sikuwapitia kuomba msaada na badala ya kunisadia wengi wao walionyesha kutaka kulala na mimi.

Nililia na ikafikia kipindi nikasema kwa nini binadamu tunakuwa hatuna huruma kiasi hiki? Niliwaza sana tena sana na baadae nikajifariji kuwa Mungu yupo na atatenda miujiza.

Hali ya mme wangu ikazidi kuwa mbaya na wakati huu nikaona kama jitihada za makusudi zisipochukuliwa haraka basi angeweza kufa muda wowote.

Nilirudi nyumbani na kuwaza kwa kina na kuona sikuwa na ujanja zaidi ya muda huu kuamua kwenda kumkubalia bwana Dan tajiri aliyeniambia kuwa kama ningetembea naye angenipa fedha za matibabu ya mme wangu.

Nilimfuata mpaka ofisini kwake na kumwambia kuwa nimemkubali alionyesha kufurahia huku akimwita dereva wake aje anipeleke hoteli moja nikamsubirie huko.

Nilipelekwa pale hotelini na kupewa funguo za chumba kimoja kilichokuwa ghorofa ya nne na kukaa mle.

Sikuwa na ujasiri wa kukaa macho makavu nikitafakari kweli kama ni mimi niliyeko mle chumbani nikimwacha mme wangu kitandani.

Kitu ambacho sijawahi kamwe kukifikiria kufanya au kukifanya lakini nilifunga macho nikiamini kuwa sasa sikuwa na ujanja zaidi ya kujitoa mhanga kumwokoa mme wangu Morgan.

Niliagiza pombe kali na kuanza kuinywa ili initoe aibu na muda mchache baada ya Dan kuja tukiwa tumekaa mle chumbani namalizia pombe ili aanze  yake nilipokea simu kuwa kwa bahati mbaya mme wangu alifariki muda mchache uliopita.

Nilipiga kelele mle ndani na nikiwa sijui nini cha kufaya na kuanza kuona ujinga nilio ufanya yaani badala ya kukaa na mgonjwa eti nipo hotel ni nani angeniamini kuwa nilikuwa natafuta fedha ya matibabu ya mme wangu??

Na je ningeuficha wapi uso wangu mimi Salome wa watu kwa aibu hiyo?????

Nikafungua dirisha na kujirusha toka ghorofa ile ya nne mpaka chini kabla ya kushtuka naanguka sakafuni kumbe nilikuwa usingizini na ni ndoto tuu.

Nikamka na kuangalia kitandani nikamwona mme angu ananishangaa na kuniuliza salome kuna nini?

Nikamsimulia hii ndoto na wote tukashia kucheka...

You Might Also Like

0 comments: