Henry bila kuchelewesha naye kamjibu"FARASI PUA YAKO"
Henry alikuwa akiendesha gari lake kwa spidi na upande wa pili wa barabara Neema alikuwa pia akiendesha gari lake kurudi uelekeo aliotoka Henry.Neema akafungua kioo cha gari lake na kumwambia Henry kwa sauti "FARASI" na Henry bila kuchelewesha naye kamjibu"FARASI PUA YAKO"
Huku akiwa karidhika na jibu alilompa Neema, Henry akaongeza sauti ya mziki, akafunga kioo cha gari lake na kuendelea na safari yake.
Mita chache mbele kuna farasi walikuwa wamemtoroka mkulima na wako barabarani mmoja wao akagongana na gari na kusababisha Henry kujeruhiwa.
Funzo
Wanaume wengi tunawadharau wanawake na kutoelewa ni nini wanajaribu kutuambia au kutufanyia katika maisha yetu na wengi twajikuta tukipatwa na majanga kama ya Hery katika familia zetu, kazi zetu na kwenye maisha ya kila siku
GOD BLESS WANAWAKE
0 comments: