Tofauti kati ya UPENDO na NDOA

12:49:00 Unknown 0 Comments

Mwanafunzi mmoja alimuuliza mwalimu nini maana ya UPENDO

Mwalimu akasema ili kulijibu swali lako nitaomba uende nje kwenye shamba la ngano na unitafutie shina moja la ngano lililozaa vyema kisha uje nalo.

Na sheria ni kuwa utaenda kulichukua mara moja tu na hutarudia tena kwenda.

Mwanafunzi akaenda shambani na alipofika akashangaa kuona kila shina la ngano limezaa vyema na kila alipolichagua hili akaona lile ni bora zaidi akajipa moyo akijua labda kuna lingine zuri zaidi akaendelea kutafuta.

Mwishowe akajikuta kuwa amezunguka nusu ya shamba na kila alipotazama kila moja lilionekana limezidi shina jingine kisha kwa uchungu akakata tamaa na kurudi mikono mitupu kwa mwalimu.

Mwalimu akamwambia, "Huu ni upendo" ... kila muda unakazana kumtafuta aliye bora zaidi ili umpende, lakini wakati unakuja kutambua hilo, tayari unakuwa umemkosa mtu huyo.

Mwanafunzi akauliza tena nini maana ya "NDOA"

Mwalimu akasema tena, ili kujibu swali lako nenda hapo nje katika shamba la mahindi na nitafutie mhindi mmoja lililokubwa na zuri zaidi.

Na sheria ni ile ile kuwa utaenda kulichukua mara moja tu na hutarudia tena kwenda.

Mwanafunzi akaenda tena akalizunguka shamba lile na alipopata mhindi uliomridhisha akarudi na kumpa mwalimu

Mwalimu akasema, sasa umefanya vyema umeweza kuja na mhindi na ni mzuri, ulipoliangalia ukalipenda na kuwa na imani nalo kuwa ni bora kuliko yote... "hii ndio ndoa"

Muda ni huu sasa kuamua kuendelea kutafuta upendo au uamue kukubali ulichonacho

You Might Also Like

0 comments: