HAKUNA ALIYEZALIWA KWA BAHATI MBAYA
Hebu chukulia mfano wa Chinedu na Osita maarufu kama Aki na Ukwa.
Wakati enzi hizo wakiwa shule ya msingi, sekondari mpaka chuoni kila mtu aliwachukulia vijana hawa kama viumbe wadogo wasioweza kuja kufanya chochote kwa maisha yao.
Hata pale walipojitahidi na kufanya vyema katika masomo yao bado walidharaulika na kuambiwa "kamwe hata kama wangefaulu vipi hakuna mwajiri ambaye angeajiri viumbe wadogo kama hao na kuwaachia ofisi waisimamie."
Aki na ukwa kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiripotiwa kusimulia jinsi ambavyo walipitia katika mapito magumu na hatimaye wakafanikiwa.
Lakini wanafunzi wale walisahau kuwa Mungu kamleta kila binadamu hapa duniani kwa makusudi maalumu na kumwandali maisha yake na kinachotakiwa ni kwa myhusika kujituma huku amkimwomba Mungu amfungulie milango yake.
Hebu waangalie leo, wanakula meza moja na malkia na wafalme, watu maarufu na hata wenye heshima zao.
Leo hii wanaingia kila sehemu ambako wengi wa wale waliowakebehi wanashindwa kufika.
Wameajiri watu wengi na wanawalipa watu ambao sasa wanawategemea wao ili waweze kuishi vyema.
Mungu ni mwema kwa sisi sote na kama utamtegemea yeye ni mwenye kukupa mafanikio nyakati zote na watu wakakushangaa.
Amini ni kwa kujituma huku ukimshirikisha Mungu wako atayabadili mapito yako magumu na kuwa mepesi
Ataondoa kila kikwazo mbeye yako na kubadilisha kuwa fursa ya mabadiliko kwako yenye mafanikio na kuwashangaza watu
Kamwe usikate tamaa na kuhofia kila unapopata majaribu omba na kumtegemea yeye naye kila kilichokosekana katika familia yako atakufanya wewe uwe wa kwanza kukipata na familia itafurahia.
Jina lako litafurahiwa na kila mtu hata wale waliokubeza hapo mwanzo.
0 comments: