heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee nani kaweka kisu na fedha chini ya mto wangu wa kulalia

17:20:00 Unknown 0 Comments



Haikuwa rahisi kuanza kuyamudu maisha yale na kwa namna moja au nyingine kila siku usiku sikuweza kulala nikiomboleza juu ya kifo cha kipenzi wangu Amina ambaye alikufa wiki chache zilizopita akiwa anajifungua mtoto wetu wa kwanza.

Sitaki kukumbuka tuliisubiriaje ile siku ya kujifungua tukiwa na furaha kuwa na mtoto wetu baada ya miaka sita ya ndoa bila ya kuwa na mtoto, lakini kumbe ilikuwa ni siku ya huzuni ambayo laiti kama ningejua nisingeisubiri kwa furaha ile. Nililia sana baada ya kuambiwa Amina kafariki na mtoto pia muda mchache baada ya kujifungua.

Sihitaji kukumbuka ila daima nitakumkumbuka Amina sio kwa uzuri wake wa sura na umbo ila kwa msimamo wake dhabiti aliouonyesha kwangu na maisha yetu kipindi cha uhai wake na hapa nadiriki kusema kamwe sitampata wakufanana nae… lala pema kipenzi cha moyo wangu AMINA 

Baada ya msiba nilirudi ofisini na siku ya kwanza pale ofisini bosi akaniita na kuniambia kuwa natakiwa nitoe stoo lita 10,000 za mafuta kwa ajili ya kupeleka site. Nikamkubalia nilipomleteas kitabu kwa ajili ya kusaini akaniambia nimpe jioni kwa kuwa alikuwa busy kido.

Nikaondoka na kwenda kuyatoa na akaja mtu mgeni kabisa machoni pangu kuyachukua mafuta hayo na gari lake, nikakataa na kumwambia ngoja nikaongee na bosi. Bosi alinitukana na kuniambia unafikiri mie naweza kuwa kichaa kukuletea mwizi?????? Mpe mafuta haraka sana… nikamwomba asaini akakataa na kusema nisimfundishe kazi.

Nikamwomba msamaaa na kuondoka haraka kwenda kumpa mafuta yale yule jamaa naye akatokomea. Maajabu ni kuwa siku ya pili yake asubuhi bosi yule yule akiwa na walinzi wa ofisi na polisi wawili wakanishika na kuniambiwa nahitajika polisi kwa maelezo. 

Kufika huko nikaambiwa natuhumiwa kwa kuiba zaidi ya lita 20,000 za mafuta ya kampuni na kuyauza baada ya kukataa akaja yule jamaa niliyempa mafuta aliyeagizwa na bosi na kuniambia kuwa mimi huwa namuuzia mafuta na nimekuwa nikifanya kwa muda mrefu. 

Sikupewa nafasi ya kujitetea na kupandishwa kizimbani na baada ya wiki tatu nikasomewa mashtaka na kuambiwa nitapoteza kazi na haki za msingi ili kulipa fidia hiyo.

Maisha yalikuwa magumu na kila siku nililia sana hasa nikiiona picha ya mke wangu na kuumia kwani nyakati za shida kama hizi alikuwa msaada wangu. Nikakumbuka baba , mama na mdogo wangu walivyokufa katika ajali ya moto na kuniacha nikiwa sina ndugu kwani walikuwa ni wakimbizi waliopata hifadhi katika kijiji nilichozaliwa.

Nikamkumbuka mke wangu ambaye naye hakuwa na baba zaidi ya mama yake tu na sasa alikuwa ni marehemu na baba aliwakimbia miaka mingi iliyopita.Nikaona dunia sasa inageuka na kuwa msumari wa moto na sijui nini nifanye niweze kuishi.

Nikafanikiwa kupata kazi katika hoteli moja, nikijishikiza kwa muda huku naangalia nini cha kufanya ingawa ilikuwa na matatizo sana. 

Baba mwenye nyumba akaanza kudai fedha ya pango nami nikawa sina ujanja nikamwomba anipe miezi miliwi nimlipe lakini wakati huo nikianza kuona dalili za kuwa kijana wa mtaani zikininyemelea kwani sikuwa na uwezo wa kulipa kwa kipato changu.

Usiku mmoa nikiwa nimelala, ndotoni akaja dada mrembo na kuniambia sasa naomba nikusaidie japo upate fedha ya kulipia pango na pia nataka uanze biashara na kujitegemea kwani mkeo aliniomba niwe msaada. Nikacheka na kusema usinikumbushe kipenzi changu, amekufa na kamwe hawezi kurudi tena wala kuwasiliana na watu wazima. 

Dada akaufungua mkoba na kutoa fedha za kimarekani dola elfu moja na kusema utalipa kodi na kulipia pango la biashara kwanza na ukimaliza niambie nini unataka kuwa biashara yako nami nitakupa hela mapema kama ukifanya mapema, nikazichukua fedha zile na kuziweka chini ya mto na kulala.

Siku ya pili nikaamka na kuanza kuikumbuka ndoto ile na nilipofunua mto nikaziona zile fedha za kigeni, nikaogopa lakini nikazichukua na kwenda benki nizibadilishe nikiwa na hofu kwani zaweza kuwa feki nami nikashikwa na kufungwa. Lakini maajabu ni kwamba zile fedha zilipokelewa na kupewa fedha za kitanzania zaidi ya milioni moja na nusu.

Nikamlipa mzee fedha yake na lakini nikahofia kwenda kuchukua ofisi, usiku nikiwa nimelala binti akanifuata na kuniambia,

“tafadhali naomba uwe mwaminifu kwani unaweza nichukia katika maisha yako, kesho nenda tafuta chumba na kulipa kama nilivyokueleza”

akanipatia namba ya kwenye karatasi ya mtaa huo ambao yeye aliopenda upenda na kisu kama ishara ya hasira zake kama nikienda ndivyo sivyo.

Asubuhi nikaichukua ile karatasi na kukiacha kisu na kisha kuanza kwenda ule mtaa, nikiwa njiani mbele yangu nikamwona binti kama yule nikaanza kumfuata nimfikie lakini aliongeza mwendo na karibu na ule mtaa akapotea.

Nikakaa chini na kuamua nirudi nyumbani bila kuulizia chumba wala kulipia, nikiwa njiani mara ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

Comment "malizia" kisha share ili niimalizie hadithi hii ya kusisimua
Whatsapp 0713317171

You Might Also Like

0 comments: