Habari ya motoooo!!!!: Binti apewa sapraiz ya mwaka ashindwa kukataa aolewa bila kutarajia..... Marafiki waandamana.....Mbeya kuna mambo walai tena

16:10:00 Unknown 0 Comments

Nakumbuka nilikuwa natoka kazini majira ya saa kumi jioni nikipa katika mtaa mmoja nikakutana na kijana mmoja akiwa kakaa kinyonge sana.

Akaniambia dada je utaweza kunisaidia japo 2000 niweze kupata chakula?

Kama ilivyo kawaida ya vijana wa mjini ambao hawapendi kazi na mwishowe kuwa omba omba nikaona isiwe taabu nikampa.

Alinishukuru sana mpaka nikajawa na huruma kidoogo nimwongeze ila akili ikanikumbusha suala la chuma ulete na baadhi ya matapeli wa mjini ambao hujifanya kuwa wanashida kumbe ni matapeli.

Kijana huyu alikuwa kama ana miaka mitatu au minne zaidi yangu na kiukweli alionekana nadhifu sana.

Ikawa haipiti siku mbili kila nikipita pale ananisalimia na muda ulivyozidi nikaona nazidi kuwa karibu naye.

Ukaribu ule uliendelea mpaka nikamkaribisha nyumbani kwangu na akawa rafiki wa karibu sana pale mtaani.

Lakini kuna jambo likawa linaniumiza kichwa juu yake kila nilipotaka kuomba niende kwake alikataa kata kata na hata kukosa raha.

Nikaanza kuhisi asije akawa sio mtu mzuri hivyo nikaanza kumwekea mitego ya kupajua kwake ili niiridhishe nafsi yangu kuhusu ukweli wa maisha yake.

Nilifanikiwa siku moja kumnasa akiwa anaelekea kwake na nikamnyemelea mpaka nilipofanikiwa kuingia kwake.

Aliduwaa kwa mshangao na hakuonyesha kupenda mtu afike pale kwani alikuwa akilala chini na chumba kilionekana kitupu zaidi ya nguo kadhaa pamoja na kagodoro kadogo, begi pamoja na kajiradio.

Hakuweza kuongea kitu na ilimchukua siku kadhaa mpaka alipokuja kunipa ukweli juu ya maisha yake.

Jina lake halisi anaitwa Morgan na aliishia kudato cha nne na kusomea udereva baada ya kukosa wa kumsomesha na hakubahatika kuajiriwa mpaka pale alipoamua kuja mjini kutafuta maisha.

Pamoja na mambo mengine ya kutoifahamu familia yake nikuta naanza kuumia na kuingiwa na moyo wa kumsaidia.

Wakati huo mimi niloajiriwa katika kampuni moja nikiwa kama secretary hivyo nikawa najaribu kumpa sapoti ya mahitaji machache na kuangalia kama ningeweza kumsaidia apate ajira.

Muda ulivyozidi kwenda nikaja kujikuta tayari nina uhusiano na Morngani na bila hata ya kushangaa nikaona upendo unazidi zaidi na zaidi ni kuwa hakuwa kijana wa makuu wala mwenye kuniomba msaada mpaka pale mimi nilipohisi ana uhitaji.

Tulizidi kupendana na wakati huo alikuwa amepata daladala ya kuendesha ingawa mimi nilikaa na kufikiri kisha nikaona ni bora nichukue mkopo pale ofisini wa milioni mbili ili nimpe aanzishe biashara.

Alifurahi sana baada ya kumpa zilefedha na siku ya pili yake ilikuwa aende kulipia chumba na kununua mzigo ili duka lake lianze kazi.

Usiku ule hakuwa mfupi kwani
niliona masaa hayaendi ili muda ufike nitoke kazini nikashuhudie duka la mpenzi wangu likiwa tayari kwani sehemu ya kuchukulia mzigo haikuwa mbali na pale hatimaye asubuhi ikafika na nikaenda kazini.

Niliwahi siku hiyo kutoka kazini na moja kwa moja nikaenda katika kilechumba cha duka na kukishuhudia kikiwa kimefungwa wazo la haraka likanijia kuwa atakuwa amechoka yuko nyumbani.

Nikapitiliza mpaka nyumbani kwake ambako niliishiwa nguvu baada ya kuona macho yakionyesha kuwa alikuwa akilia na pia nguo yake imechanika.

Nilichoka na hata sikitaka kuuliza kitu zaidi ya kumwambia pole... Akaitikia ki shingo upande na kunisimulia kuwa alivamiwa akiwa anaelekea kulipa pango ili aende mjini kununua mizingo ya duka.

Nilimwelewa na ikapita miezi kama mitano hivi tukiwa tunashirikishana mipango ili tujue tutaishije na wakati huu sasa akawa amepata kazi ya kuendesha gari la watoto wa shule moja pale mtaani na tukawa tunaishi kwa furaha kila mtu akimpenda na kumwamini mwenzake na kuwa tukijiweka vyema tutaanza taratibu za ndoa.

Siku moja nikiwa kazini nilipigiwa simu na rafiki yake Morgani kuwa morgan amepatwa na ajali na hivyo amesafirishwa kupekekwa makao makuu ya mkoa ambayo yalikuwa umbali wa takribani kilomita 300 na kitu kutoka pale tulipokuwa na hivyo anakuja kunichukua twende haraka.

Nikatoka ofisini baada ya kuomba ruhusa na kwenda mpaka nyumbani ambako nilichukua akiba ya fedha na wakati huo fred alikuwa kaja na gari pale.

Aliendesha gari lile na baada ya masaa matano tulifika pale na muda huo ilikuwa ni saa kumi na moja ya jioni na gari likaingia hospitali moja kubwa pale.

Alikuja mtu kutupokea na kutupeleka chumba kimoja lakini chumba hiki kilikuwa kama ni ofisi vile na dada mmoja akaja akitaka kutupa kahawa.

Nilikataa kwa kuwa nisingeweza kula au kunywa chochote bila kujua morgan wangu anaendeleaje..... Hivyo dada akaondoka.

Robo saa baadae alikuja dada mmoja aliyevalia kama ni secretary akatuita kuwa tunaitwa na boss wa hospital..... Wakati huo machozi nilishayafuta zaidi ya mara sita na sasa kwikwi zilianza kwa chinichini nikiamini tunaenda kupokea taarifa za msiba wa kipenzi changu Morgan.

Ulifunguliwa ule mlango mwili ulichoka pale nilipokutana uso kwa uso na Morgani akiwa amekalia katika kiti cha mkurugenzi na kabla hata sijatamka neno nilishangaa kuona picha za mimi na yeye zikiwa mle ofisini.

Nilishindwa kuongea wala kusema kitu zaidi ya kuishiwa nguvu na baada ya kusaidiwa kunyanyuka nililala usingizi mzito na kuamka siku ya pili yake.

Niliamka na kushangaa nipo kwenye jumba la kifahari na wafanyakazi wakiniita mama, nikauliza hapa ni wapi wakaniambia ni nyumba ya Morgani..... Nilishangaaaa

Morgani wakati huo alikuwa ameondoka na aliporudi alikuwa yuko na wazazi wake na ndio wakaanza kunisimulia kisa cha mimi kudanganywa kuwa morgan ni kijana fukara.

Morgani anatoka katika familia ya kitajiri sana pale jijini na katika maisha yake kila mwanamke aliyekuwa nae kwenye mahusiano hakuwa na mapenzi zaidi ya fedha..... Baaada ya kuumia vya kuyosha akaja na wazo la kwenda mbali na kujifanya maskini na kisha kunipata mimi na anahisi kwa zaidi ya mwaka na zaidi tulioishi wote nafaa kuwa mke.

Siku ya pili yake alinipa ile fedha aliyosema imeibiwa na nikafanya utaratibu wa kuacha kazi na kuhama kule kijijini na sasa naitwa mama morgan na wengi wanapenda kuniita salome morgan

Na niliolewa kwa namna hii na sasa nina miaka 6 ya ndoa........... Share nawe story yako.

You Might Also Like

0 comments: