Ishi kwa upanga utakufa kwa upanga........ Kisa cha kweli
Nimeichukua mahali ila ila somo zuriKuna Hakimu anaitwa Godson, siku moja alipokuwa ndani ya gari lake akipita sehemu Fulani usiku alishuhudia kwa macho yake John akimuua Selemani kwa kumpiga na shoka kichwani. Hakimu Godson alishtuka sana lakini hakuwa na kitu cha kufanya kwa sababu John alikimbia.
Baada ya siku kadhaa, kesi ikafikishwa mahakamani, katika mahakama ambayo Hakimu Godson hufanya kazi. Kesi ile ilikuja kwa aina tofauti sana, mtu ambaye alikuwa akishikiwa kwa mauaji ya Selemani hakuwa John bali alikuwa Andrew.
Hakimu Godson akachanganyikiwa. Alijua fika kwamba Andrew hakuua bali aliyeua alikuwa John ambaye kwa macho yake alimuona akitenda kosa hilo na kukimbia. Godson akapata wakati mgumu mno, hakujua afanye nini kwani hata kuwa shahidi hakuweza.
Alipoona kwamba mambo yamekuwa magumu kwake, akaamua kutaka muda wa mapumziko na wazee wa baraza na kisha kuelekea ndani ambapo akatafuta chumba huku akimtaka Andrew afike ndani hapo mara moja.
Andrew akafika, uso wake ulionekana kuwa na wasiwasi mwingi mno, akamwambia akae kwenye kochi huku ndani ya chumba hicho wakiwa wawili tu.
"Ninajua kwamba haujafanya mauaji, aliyefanya mauaji ninamfahamu kwa sababu nilimuona kwa macho yangu," hakimu Godson alimwambia Andrew.
"Huo ndio ukweli hakimu, sijaua, sijaua kabisa, sijamuua Selemani," Andrew alisema huku akilia.
"Sawa. Naomba nikuulize swali. Hivi ulikwishawahi kuua katika maisha yako?" aliuuliza hakimu Godson, swali hilo likamfanya Andrew kuanza kulia. Alichukua muda mrefu kulia, aliponyamaza, akauinua uso wake na kumwangalia hakimu usoni.
"Ndio niliwahi kuua ila hakukuwa na mtu aliyeniona," alijibu Andrew.
Hakimu Godson hakutaka kusikiliza kitu kingine chochote kutoka kwa Andrew, alichokifanya, akamhukumu kunyongwa.
LENGO LA KUKUAMBIA HILI
Andrew alifanya mauaji na wala hakuonekana, Mungu anaona, unapofanya kitu kibaya, hauhukumiwi hapo hapo, wakati mwingine huchukua muda mpaka kuhukumiwa.
Andrew alihukumiwa kwa kosa alilolifanya miaka ya nyuma na si lile lililotokea. Unapomfanyia mtu ubaya, haulipiwi ubaya peponi au motoni, ubaya utalipwa hapa hapa duniani hata kama ni kwa staili nyingine tofauti na unayoitegemea.
Ukitenda mema leo, Mungu atakulipa hapa hapa, haijalishi utapewa na nani au utapata kutoka kwa nani, bado utalipwa hapahapa.
like Tabasamu na Fuledi
0 comments: