ISOME MPAKA MWISHO HAKIKA MAPENZI SI MCHEZO
Mimi na girlfriend wangu tulikuwa tunapendana sana.
Tulikuwa tumeishakuwa pamoja kwa muda wa miaka minne hivi, na hivyo tukaamua tuoane.
Ila kulikuwa na jambo moja dogo lililokuw alikinisumbua sana, nalo si linguine bali ni mdogo wake wa kike ambae kiukweli alikuwa mzuri
sana.
Huyo binti (shemeji yangu) alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja
hivi, na muda wote alipendelea kuvaa sketi fupi fupi na fulana
nyepesi au brauzi zinazoonesha mwili wake.
Na kwa jinsi kifua chake kilivyo alikuwa hahitaji kuvaa sidiria, naamini unapata picha ya mtu
nnayejaribu kumzungumzia.
Pamoja na binti huyu kuwa
mwembamba kiasi, alikuwa na umbo la ajabu, yaani kiuno chake
kiliumbwa mithiri ya nyingu mweusi.
Tatizo ni kwamba mara nyingi binti alipokuwa akiniona alikuwa na tabia ya kujipitisha pitisha na
kuinama mbele yangu ili kunionesha mtaji wake.
Kusema kweli nilikuwa navutiwa sana na uzurivwake, na pia nilijua
alikuwa ananifanyia makusudi maana alikuwa hafanyi hivyo kukiwa na watu wengine, bila shaka
alikuwa ananitaka.
Siku moja binti huyo alinipigia simu niende nyumbani kwake nikaangalie kadi za mialiko ya harusi alizokuwa amechapisha,
nilipofika (wakati naingia
ndani) akaninong'oneza kuwa ananitamani sana na kamwe hawezi kujizuia.
Akaendelea kunieleza kuwa anahitaji tufanye mapenzi kabla sijafunga ndoa na dada yake ili nisijisikie vibaya kwamba natoka nje ya ndoa.
Nilipatwa na bumbuwazi na hasa kutokana na nguo za nusu uchi
alizokuwa amevaa.
Kabla sijamwambia lolote akaniwahi na kusema "Mimi
natangulia juu (ghorofani) kwenye
chumba changu, kama unahitaji nikupe kitu kitamu njoo haraka
kabla mashetani yangu hayajapoa" akageuka na kukimbilia chumbani.
Haraka nikageuka na kuelekea mlango mkubwa wa kutoka nje
kutaka kuelekea kwenye gari yangu.
Daaah...! Kwa mshangao mkubwa nikaona pale nje familia yote imekusanyika, waliponiona nikitoka
wakanipigia makofi na vigelegele kwa furaha, huku wengine machozi
yakiwatoka kwa furaha.
Baba mkwe akaniambia
"Tumefurahi sana kwamba umeshinda mtihani mdogo wa
uaminifu ulioandaliwa na familia. Ila kiukweli unajua ni nini hasa kilikuwa kinafata...?
Ukweli ni kwamba MDA ULE NATOKA KULE NDANI NILIKUWA NAENDA KWENYE GARI KUCHUKUA CONDOM…!
0 comments: