Siasa ni kumzidi mwezio kete katika kupanga maneno tuu na wananchi wao hukubali chochote na kubadilika kulingana na utamu wa maneno

08:35:00 Unknown 0 Comments

Siasa ni kumzidi mwezio kete katika kupanga maneno tuu na wananchi wao hukubali chochote na kubadilika kulingana na utamu wa maneno

Mbunge mzee na kijana walikuwa wanagombania ubunge katika jimbo moja. 

Wakakutanishwa ili wamwage sera kwa wananchi na mshindi apate ubunge......

Kijana: Jamani mimi ni kijana na naomba mnipe nafasi nimsaidie huyu mzee maana kachoka na anahitaji kupumzika sasa.

Wananchi: umepitaaa

Mbunge mzee: Ndugu zangu wa jimbo hili wote nyie ni wanywaji wa ulazi:

Wananchi: Ndiooooooo

Mbunge mzee: je mnapenda ulanzi uliokomaa au mtogwa?

Wananchi: uliokomaaa

Mbunge mzee: Basi mimi nimekomaa naomba mnipe nafasi tena nionyeshe ukomavu wangu zaidi

Wananchi: Umepitaaaa

Kijana: Jamani wanachi huyu mzee sikakaa kwa vipindi viwili??

Wananchi: Ndioooooo

Kijana: Kipindi cha kwanza kajenga nyumba mjini na kipindi cha pili kajenga nyumba hapa kijijini... Sasa anaomba kipindi kingine ili awafilisi zaidi?

Wananchi: Fisadi asipite tena huyoio

Mbunge mzee: Ndugu wananchi, ni kweli kabisa. Kipindi cha kwanza nilijenga nyumba mjini na sababu ni kwamba kukaa nyumba ya wageni niliona ni gharama mmo, hivyo nikaamua nijenge nyumba ambayo nitakaa na wasaidizi wangu nikiwa bungeni kupunguza gharama ili fedha zisaidie kazi za mandeleo.

Wananchi: Uamuzi wa busaraaaaa

Mbunge mzee: Na kipindi cha pili nikaona nijenge nyumba nzuri na ya mfano hapa kijijini ili na wananchi wapate hamasa kutoka kwangu ndugu zangu. Na sasa naomba mnipe nafasi kwani huu ndio muda ambao nitatumia kuwatumikia kwani mjini sitakuwa na gharama na hapa nimewapa hamasa mpya ya ujenzi wa makazi bora.

Wananchi: Asante mbungeeeeeee

Mbunge mzee: Sasa naomba mnipe kura kwani mkimpa huyu kijana naye itambidi ajenge nyumba mjini na tena hapa kijijini.

Wananchi: Upiteeeee wewe kijana majangaaaaaaa

Wewe ungemchagua yupi kati ya hao?

You Might Also Like

0 comments: