Jinsi kifo kinavyoweza kukuita na kwa kiburi ukakifuata bila kusoma alama za nyakati
John aliamka jumamosi akiwa na hamu ya kwenda kuogelea bwawani ingawa kila rafiki aliyemtaka waende wote alishindwa kutokana na kubana na kazi.
Akaichukua baiskeli yake na kuanza safari ya kwenda bwawani akiwa na hamu ya kuogelea siku hiyo.
akiwa njiani tairi la nyuma la baiskeli lika pasuka hivyo akalazimika kurudi na kuliziba tairi lile na baada ya kuliziba akaanza safai ya kuelekea bwawani
Alipofika sehemu ile ile tairi la nyuma lilikobasi tairi la mbele nalo likabasti na akalazimika kurudi tena kwa fundi baada ya kujiridhisha kuwa hakukua na msumari wala mtu uliosababisha ajali ile.
Akaliziba tairi lake na kuendelea na afari yake lakini alipofika ile sehemu tena spoko 10 za tari la nyuma zikakatika na kufanya asimame na kurudi kwa fundi huku akijiuliza ni balaa gani lipo eneo lile bila ya majibu?
Kwa fundi akaazima baiskeli nyingine na kwenda na mara hii akafika bwawani na kuanza kuogelea.
Akiwa katika kati ya kwenye maji ghafla akakosa nguvu na kuzama na walipokuja kumwokoa tayari alikuwa katika hali mbaya na alifariki njiani kaba ya kufika hospitalini.
Funzo
Kupitia habari hii tunajifunza jinsi tunavyopewa viashirio vya kuwa tunakoenda kuna weza kuwa na matatizo lakini nasi twazidi kujipa kiburi na kutumia uwezo wetu wa kifedha au ubavu kujipeleka kwenye matatizo.
Kila mtu ana namna ambavyo huepushwa na mambo mengi na hii haiji bure bali huwa ni njia ya Mungu wetu kutuepusha katika mambo mhatarishi katika maisha yetu.
Ni vyema katika baadhi ya vitu ukipata ishara kamam hizi kujikabidhi kwa Mungu huku ukiomba ulinzi wake kwa jambo hilo
Kwa wanaomtegemea Mungu katika kila jambo na kuomba ulinzi wake katika kila ishara mbaya ruka ku-comment neno Amen na kisha share ujumbe huu
0 comments: