Je, umechana na mpenzi wako? Haya hapa mambo 10 ya kuzingatia unapotaka kuanzisha mahusiano mapya

15:53:00 Unknown 0 Comments

kuachanaKutengana na mpenzi si jambo ambalo wanaadamu huwa tunalipendelea, lakini pia ni ukweli tusioweza kuupinga kwamba, haya ni miongoni mwa majaribu ambayo tumeumbiwa wanaadamu na ambayo hatuwezi kuyakwepa.
Mara nyingi, kwa kuzingatia ukweli kuwa kutengana na wenza wetu haimaanishi kupoteza uwezo wetu wa kuwa na mwenza mwingine, ni wazi kabisa kuvunjika kwa mahusiano yaliyopo mara nyingi humaanisha kuanzisha na hatimaye kujenga mahusiano mapya. Lakini je, unajua ni mambo yepi ya muhimu ambayo unatakiwa kuyazingatia wakati unapokuwa unakabiliana na maumivu ya kuachana na mpenzi wako wa awali huku ukiwa unatafuta kuanzisha mahusiano mapya?
Kwa msada wa mashirika mbalimbali ya habari na mitandao, hapa ni mambo kumi ya kuzingatia unapokuwa katika kipindi hiki cha mpito:
1. Rejesha/Boresha mawasiliano ndani yako:
Kabla hujachukua hatua ya kuanza mahusiano mapya, ni vyema kwanza ukajitizama upya. Ni wazi kabisa kuwa katika kipindi cha mahusiano fikra zetu kwa kawaida zinakuwa zimeelekezwa zaidi katika kuwasikiliza wenza wetu. Ile hali ya mtu kujisikiliza mwenyewe kihisia huwa inakuwa haipo. Hivyo basi, inapotokea umeachana na mwenza wako, kabla hujaanza mahusiano mapya, ni vyema ukarejesha ile hali ya mawasiliano ndani yako kwanza. Hili litakufanya ujitambue kuwa uko kwenye hali gani kihisia, namna gani ya kujiandaa na aina gani ya mahusiano ambayo unataka kuanzisha.
2. Tengeneza marafiki walio single:
Ndio. Mara nyingi tunapokuwa kwenye mahusiano, bila sisi wenyewe kujua, hujikuta tukiwa na marafiki ambao nao wako na wenza wao. Ni mara chache sana huwa tunabakia na marafiki walio single, na tunapokuwa nao wanakuwa ni wachache sana pia.
Huu unakuwa wakati mzuri wa kurejesha marafiki walio single kama wewe. Hili litakusaidia kuyaona maisha rahisi kwani kujichanganya na marafiki walio single kunakuwezesha kung’amua fursa nyingine zilizojaa duniani ambazo ilikuwa vigumu kuziona wakati ulipokuwa kwenye mahusiano. Wataalamu husema pia huu ni wakati mzuri wa kurejesha ile hali ya kujiamini na kujiendeshea maisha kama mtu uliye single, kwani kihulka, kuna kiwango kikubwa cha mtu kujiamini kinapotea wakati unapokuwa kwenye mahusiano. Aina hii ya marafiki pia inakuwezesha kupata mbinu mpya za kuanzisha mahusiano kulingana na mazingira ya singles waliopo wakati huo, kwani hawezi kuwa sawa na hali ilivyokuwa wakati unaanzisha mahusiano yako ya awali
3. Usiwe na haraka
Ndio, ukweli ni kwamba, kwa wakati huu uko peke yako baada ya mahusiano ya awali kuvunjika. Sasa una harakisha wapi? Kitaalamu, kama unajihisi kuwa bado unajihisi hali fulani ya hasira kwa kuvunjika kwa mahusiano yako ya awali, basi ni vyema ukajitambua kuwa hujawa tayari kuanzisha mahusiano mapya.
Ikiwa huwezi kuzungumza kuhusu mtu mliyeachana kwa hali ya kawaida, kwa maana unazungumza bila kumzungumzia mpenzi wako wa awali kama mtu mwenye hatia, aliye na makosa nk, basi subiri, kwani ni rahisi kuangukia mikononi mwa mtu ambaye atataka tu kutumia matatizo yako kuku-win na sio kwasababu ana mapenzi ya dhati na wewe.
4. Kuwa mwepesi kuomba msaada wa kiushauri
Ndio, mara nyingi sana mahusiano yetu yanapovunjika, ni mara chache sana ambapo utamsikia mtu akikiri kuwa alikuwa chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano hayo. Mara nyingi, kila upande huishia kutupa lawama kwa upande wa pili kama sababu ya kuharibika kwa mahusiano yoyote yale. Sawa, inawezekana kweli kuwa upande wa pili ulihusika katika kuharibikiwa kwenye mahusiano yako, lakini je, ni nani alikwambia kuwa wewe ni malaika?
Tafuta ushauri, ongea na watu wengi kwa kadiri unavyoweza na usiwe mnyonge katika kuweka wazi kile kilichotokea katika mahusiano yako yaliyotangulia, ukijieleza kwa kufuata kanuni ya tatu hapo awali.
Fanya pia tafiti kuhusu mahusiano ya watu mbalimbali, iwe kwa kuangalia jamii inayokuzunguka, au kupitia sehemu mbalimbali kwa njia za mitandao.
5. Usijilaumu au kujihisi vibaya ikiwa mambo hayaendi sawa
Jijasirishe kwa kuuweka ubongo wako kwenye hali ya kukubali kuwa, kuanzisha mahusiano mara nyingi haimaanishi kuwa mambo yatakwenda kama tunavyokuwa tunayapanga kichwani. Ni vyema kutambua kuwa, kuanzisha mahusiano ni mchakato au zoezi ambalo kama tukilichukulia kuwa linaweza kuwa na matokeo hasi pia, basi huenda ikakusaidia kupunguza sana maumivu au hali ya kujihisi kukosa amani pindi inapotokea pale tulipotaka kuangukia hapajawa sahihi.
6. Fake It ‘Til You Make It.
Ndio, hii ni kanuni moja muhimu katika kukabiliana ukweli hasa pale mambo yanapokuwa magumu. Tumeshazungumzia awali kuwa katika mazingira kama haya, baadhi ya watu hupoteza hali ya kujiamini, na hali hii huenda ikamgharimu mtu katika kuanzisha mahusiano mapya. Unaweza kukuta muda unaenda huku kila ukiwaza kujaribu kufanya move, unakuta moyo unasita. Hapa ndipo mahali muafaka kufanyia kazi kanuni ya “fake it ’til you make it”.
Wataalamu husema kuwa, hali ya kujifanya unajiamini, mara nyingi humfanya mtu kutenda jambo katika hali ya kujiamini zaidi ya anapokuwa anajiamini kwa kawaida. Licha ya hayo, wataalamu pia wanabainisha kuwa kujifanyisha jambo mara nyingi ndio mwanzo wa kukihisi utamu wake na ukakifanya kwa uhalisia badala ya kujifanyisha tu. Mchambuzi mmoja wa mahusiano, Malkin, aliwahi kuiandika hali hii kwa lugha ya kiingereza akisema “First we act; then we feel.”
7. Usikimbilie kukusanya taarifa za kina haraka haraka:
Mtu unayetaka kuanzisha mahusiano naye anatakiwa akuone wewe katika gamba lako wewe mwenyewe. Kimsingi kama unakuwa umejipa muda wa kutosha, hili linawezekana kabisa. lakini hata kama hujajipa muda wa kutosha, basi zingatia hili.
Battista, mmoja wa waandishi mahiri wa makala zenye kuhusiana na mahusiano yaliyokwenda harijojo, anasema kuwa, si vyema kukimbilia kuufunua ukweli kuhusu mahusiano yako ya awali, ili kumuwezesha mtu wako mpya kukuchukulia katika gamba analokuona nalo ukiwa mbele yake, na sio umpe nafasi ya yeye kuwa na picha fulani ya moyo wa mtu ambaye awali ulishajeruhiwa.
8. Jipe nafasi ya kutokuhamanika kwa mara ya kwanza
Ndio, mara nyingi huwa ile outing ya kwanza ina presha zake na wengi wetu ama hujikuta tumechemsha au kujikuta tumekuwa kituko huku tukija kujutia baadae. Hili ni jambo la kiasili na wala hutakiwi kuliona kama udhaifu hata kidogo. Kwa kutambua hili basi, ni vyema ukajipa muda wa kujishusha aina yoyote ya shinikizo ambalo unalihisi ndani yako pale unapokuwa unajiandaa kwa mtoko wa kwanza na mtu wako mpya.
Kila zinapokujia fikra za shinikizo kuhusu mtoko wako wa kwanza, jipe muda wa kutosha kukabili hali hiyo. Vuta pumzi za kutosha kwa dakika kadhaa, kunywa maji mengi ya kutosha na jenga mazoea ya kufikiria itakuwa vipi kama mambo yakienda sawa na ulivyopanga wewe, badala ya kuwaza itakuwaje ikiwa mambo yasipoenda sawa. Hili litakuongeza ujasiri zaidi
9. Usihofie kukabiliana na matokeo mabaya
Ndio, mara nyingi uanzishwaji wa mahusiano mapya huweza kuishia kwa matokeo mabaya ambayo hatukuweza kuyatarajia. Na hili mara nyingi hutujaza hofu kubwa sana. lakini je, kuna jambo baya katika mahusiano ambalo unadhani litakuumiza kama mahusiano yako ya awali ambayo yamevunjika? Ukweli ni hapana, sasa basi kwanini uhofie kuwa kutakuwa na baya zaidi ya hapo?
Jipe ujasiri, kabiliana na hiyo hali. Bila kujali kuwa matokeo yatakuwaje, ingia ukiwa na dhamira ya kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuanzisha mahusiano mapya unayotaka kuyafurahia. Matokeo mabaya na mazuri huwa ni sehemu ya maisha na changamoto ambazo huenda zikaishia kukufanya uwe mtu imara zaidi ya ulivyokuwa ukijidhania.
10. Usiyachukulie mambo serious
Usishangae. Ni kweli kwamba uko katika harakati za kuanzisha mahusiano mapya baada ya yale ya awali kutokwenda vizuri, lakini haishauriwi uanze kuyachukulia mambo serious toka siku ya kwanza. Ni vyema kuyapa mahusiano mapya nafasi ya kuchanua kwa njia ya utani utani zaidi kuliko kuanza nayo kwa kuyachukulia serious.
Jitengenezee muda wa kuichunguza na kuitathmini kila hatua unayopita kabla ya kuingia hatua inayofuatia
Asante kwa jukwaahuru.com

You Might Also Like

0 comments: