Mabinti wa mbeya duuuh, mnatisha
Nimekutana na mabinti makomandoo ila huyu wa leo katisha......
Naelekea sehemu kupata supu nikaona meza moja wamekaa, nikaomba kama naweza kukaa nao lakini hakuna aliyeongea.
Basi nikakaa na kuagiza zangu nikishushia na ndovu yangu, kaja jamaa achukue bill nikatoa kimfuko kina minoti kibao ( ada ya mwanagu).
Yule dada aliyekuwa na kiburi kuona wale wekundu bila aibu akasema " dadii!!!! dadiii!!!! dadiii!!!, inzi atadumbukia kwenye glass yako tumia hii kufunika glass yako dadii"
Yaani nimeishiwa nguvu.... aki ya nani mbeya kama dar vile

0 comments: