Mama wa ajabu huyu.. Ona alichomwombea mwanae "ninakuombea kwa Mungu, ukirudi mjini ugongwe na gari kubwa zaidi ya lile la mwanzo"
Kijana mmoja aitwaye Mtafya alienda kutafuta maisha mjini.
Alipofika huko akawa mwigizaji na kipaji chake kikazidi kukua huku akipata umaarufu mkubwa sana kwa mashabiki na waigizaji wenzie pia.
Siku moja aliigiza katika filamu na kupewa scene ya kugongwa na gari dogo na kufa papo hapo.
Filamu ile ilipata umaarufu sana na kuuzwa mpaka kijijini na mama wa mtafya akahuzunika na kuomboleza sana akijua mwanae kafa kiukweli baada ya kuitazama filamu ile.
Baada ya kimya kirefu mtafya akaamua arudi kusherehekea siku kuu ya mwaka mpya kijijini kwake na mama yake.
Mama aliogopa alipomwona akijua ni mzimu lakini baada ya kueleweshwa na kupewa zawadi nyingi na fedha akafurahi sana na
wakasherehekea sikukuu salama.
wakasherehekea sikukuu salama.
Wakati mtafya anajiandaa kurudi mjini kwenda kuendelea na mwaka mpya na mipango mipya.
Mama akasali na kumwombea kwa Mungu akisema,
"Mwanangu mtafya ninakuombea kwa Mungu, ukirudi mjini ugongwe na gari kubwa zaidi ya lile la mwanzo ili uje na zawadi nyingi zaidi mwakani muda kama huu Amen"
Nami nakuombea rafiki wa fuledi mwaka huu uendelee kupatwa na baraka nyingi katika kazi zako, familia yako, afya yaKo, masomo yako na mengineyo mengi, shetani na wenye roho mbaya wakushindwe na kukuogopa.
Comment AMEN kama waamini kuwa Mungu amekupa na ataendelea kukupa mafanikio na mwaka huu uendelee kuwa na furaha, mafanikio na amani kwako

0 comments: