Mambo 31 yanayokuonesha kuwa sasa umri umeenda....

16:06:00 Unknown 0 Comments


1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi


2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani


3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe


4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini


5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala


6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa


7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye harusi, vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club


8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei


9. Idadi ya t-shirt na jeans inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo


10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu Polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua


11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako


12. Hukumbuki tena Azam IceCream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi


13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu


14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwalisha makombo


15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana


16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala


17. Ukiwa nyumbani unaanzakutumia muda wako wa ziada kulimalima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura


18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh. ngapi?"


19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba


20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Guardian, Daily News, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani


21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati


22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"


23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati


24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa


25. Ukimwona rafiki yako ana ujauzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"


26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja


27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako


28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei, na mfumo mbovu wa utawala


29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi


30. Kwa wanawake utaanza kuona vijana wanakukimbia na kwa wanaume utaanza kuona vibinti vinakupapatikia sana. 


31. Utaanza kuona aibu kuvaa mlegezo.....Ukiona una robo ya sifa hizi 31 basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma.....

You Might Also Like

0 comments: