(Mbinu mpya ya wezi kuiba jijini dar)

18:37:00 Unknown 0 Comments


Hawa wana PHD ya wizi kwa kweli......ilikuwa
hivi......mara baada ya kumaliza sherehe za
harusi katika ukumbi wa JKT MGULANI
nikatembea kwa mguu hadi kituo cha daladala
si unajua tena sina gari, nilipofika kituoni
ikapita haice na waliponiona konda aakasema
unaenda wapi nikamjibu kariakoo basi
nikafunguliwa mlango na kuingia na kukaa
kwenye siti na kulikuwa kuna abilia saba,
mara naambiwa oya tupo kazini hapa tena
vyetu, mimi nikajua nauli nikatoa miatano ili
nilipe, mara nikatolewa panga na mwingine
akatoa bastola na kusema nitoe fedha zote
nilizonazo na niwape simu, kiukweli nilikuwa
sina jinsi kabisa kwani nilikuwa kwenye kumi
na nane zao, nikawapa simu na vijihela nilivyo
navyo na wakanisachi ili kuhakikisha kuwa
hawaniachi hata na senti moja, walipolidhika
wakasimamisha gari, ila mmoja akasema si
tumpe hata alama kidogo, basi nilimwomba
Mungu na kwa bahati nzuri wakanishusha na
wakaondoka zao, kwa kuwa sikuwa na fedha
tena basi nikatembea tu kurudi nyumbani,
usinicheke rafiki yangu ila comment kunipa
pole kwani wezi si watu wazuri kabisa kwa

Chanzo kutoka kwa Deo Julias

You Might Also Like

0 comments: