Mpenzi wangu kaniambukiza UKIMWI makusudi

18:10:00 Unknown 0 Comments




Mimi ni msichana mwenye miaka 28 mwaka juzi nilikutana na kijana mmoja ambaye tukapendana na kuamua kuwa pamoja.

Wazazi walinikuwa wagumu sana kunikubalia niolewe na kijana huyo kutokana na kuwa walipata taarifa ya kuwa hakuwa ametulia.

Mimi nikamwomba tukapime na baada ya mvutano siku moja akaniambia twende tukapime ikanibidi nifuatane naye mpaka kituo kimoja na tukapima na tukaonekana kuwa wote hatuna maambukizi.

Muda mchache baadae nikawa mjamzito na mpenzi wangu akanipeleka kwenye kituo kile kile tulichopimia na nikaanza klinki na vipimo vikaonyesha sina maambukizi yoyote.

Siku zilivyokaribia za kujifungua nikaenda pale na ikasemekana ya kuwa ilinibidi nifanyiwe upasuaji kwani nyonga yangu ilikuwa ndogo.

Nikahamishiwa hospitali nyingine na na baada ya kufanyiwa upasuaji salama nikabahatika kupata mtoto wa kike.

Ila cha kushangaza ni pale nilipozuiliwa kumnyonyesha mwanagu na kuambiwa nilitakiwa kuanza kuhudhuria kupata elimu juu ya kuishi na mwanangu huyu na kwa kuwa nilikuwa na mambukizi ya viruzi vya ukimwi.

Kweli nilipokea habari hizi kwa mshtuko nimekuwa nikidhohofika kila siku na sasa ni mwaka tangu janaga hili.

Lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa nimeanza kupata habari kuwa huyu mme wangu alikuwa na maambukizi haya kwa muda mrefu.

Kitu ambacho najiuliza ni kuwa je wakati napimwa kulikuwa na mchezo unafanyiaka ama kuna nini kinaendelea kwani mimi nimekuwa binti wa kujiheshimu na kuiheshimu ndoa yangu...

Naombeni japo mnifumbue macho.


You Might Also Like

0 comments: