Msomaji wa Tabasamu na Fuledi makini ila mwenye hasira aamua kuishambulia blog hii bira huruma yaani.

Raha ya facebook bhana uwe na watu wa ukweli, ili ukiwa na majonzi wakufariji, ukiwa na huzuni wakupe furaha, ukiwa umechoka basi wakupumzishe, ukiwa mpweke wakuondolee upweke, ukiwa na stress pia waziondoe, ukiumwa tu wakupe faraja kiasi kwamba ujikute unapona kabla hata ya kumwona daktari na ukilazwa ujikute unapata nguvu ya kuingia fb, ukiwa huna imani basi unapewa imani ya kumjua mungu, ukigombana wakupatanishe na ukikata tamaa ya maisha basi wakutie moyo na kujiona alaaa kumbe bado naweza kufanikiwa, nina marafiki nawapenda sana kwa kweli. ila kuna mtu mmoja akiwa rafiki yako Fred Kihwele basi ni kama unamarafiki wote wenye kukugusa katika kila sekta ya maisha yako na ukilike page yake ya Tabasamu na Fuledi ndio balaa zaidi kwani dah!! utaenjoy, utaelimika na hata siku moja hutakasirika kwamba kuna vitu siyo vya maadili.

0 comments: